Tuesday, October 10, 2017
ZIJUE NJIA KUMI (10) NAMNA YA KUPATA WATOTO MAPACHA
watoto mapacha hupendwa sana na wanawake wengi wanaotaka kujifungua siku za usoni, lakini ni mara chache sana mwanamke kubeba mimba za mapacha.
tafiti zinaonyesha kwamba uwezekano wa mwanamke mmoja kubeba mimba ya mapacha ni 3% na kuna njia mbalimbali zinaweza kuongeza uwezekano huu mpaka asilimia tano au kumi na...
tutaziona hapo chini.
kwenye ulimwengu huu wa maisha magumu wanawake wengi hupenda kuzaa mapacha mara moja tu wa jinsia tofauti au jinsia moja na kufunga kizazi.
japokua watoto mapacha wanapendeza sana na kufurahisha nyumba sio wanawake wote wanapenda watoto mapacha na mapacha hubeba hatari kubwa kipindi cha ujauzito kwani sio rahisi kuwazaa kwa njia ya kawiada huku wakiongeza dalili za ujauzito kua kali zaidi kama kutapika sana, kuchoka sana na kadhalika.
watoto mapacha wanatokea vipi kwenye kizazi? kuna aina mbili za watoto mapacha..
mapacha wa kufanana au identical twin; hawa ni mapacha ambao hutokea pale yai la mwanamke lililorutubishwa na na mbegu ya mwanaume linapogawanyika na kutengeneza watoto wawili, watoto hawa hufanana kwa kila kitu yaani sura,tabia mpaka jinsia na hua ni vigumu sana kuwatofautisha kwa macho.
mapacha wasiofanana au non identical twin; mapacha hawa hutokea pale mayai mawili ya mama yanavyorutubishwa na kujishikiza tofauti kwenye mfuko wa uzazi, mapacha hawa hua wako tofauti kwa sura, jinsia na hata tabia..hawa ni kama ndugu waliofuatana tu.
je unawezaje kupata watoto mapacha?
kiukweli hakuna njia ya moja kwa moja ya kupata watoto mapacha lakini kuna baadhi ya sababu zinaongeza nafasi kubwa ya kubeba mimba ya watoto mapacha na tafiti nyingi zimeonyesha kwamba matumizi ya njia hizo yanaongeza nafasi kubwa sana ya kubeba watoto mapacha.
chagua mpenzi wa aina hiyo;
kama unatoka familia ambayo mapacha wanazaliwa mara kwa mara uko kwenye uwezekano mkubwa wa kuzaa mapacha na kama ukizaa na mtu ambaye kwao kuna mapacha wa mara kwa mara basi na wewe una nafasi kubwa ya kuzaa mapacha..hii ni njia ngumu kidogo kwani sio rahisi kujua utampenda nani maishani mwako..kumbuka ni mwanamke tu, aliyetoka kwenye ukoo wa mapacha anaweza kuongeza nafasi ya kuzaa mapacha, mwanaume wa mapacha hawezi kuongeza nafasi ya kumpa mwanamke mimba ya mapacha.
zaa umri ukiwa umeenda kidogo;
mwanamke akifkisha umri wa miaka 35 na kuendelea kunatokea mabadiliko ya mfumo wake wa uzazi kiasi kwamba mwili wake huanza kuachia mayai mawili kila mwezi badala ya yai moja kama ilivyokawaida, na hii huongeza nafasi kubwa sana ya yeye kubeba mimba ya watoto mapacha.
matumizi ya dawa za uzazi;
kuna dawa ambazo hutumiwa na wanawake ambao wanashindwa kubeba mimba, dawa hizi hufanya yai zaidi ya moja kuachiwa kutoka kwenye mirija ya uzazi na hii huongeza uwezekano mkubwa wa kubeba mapacha, na wanawake wanaotumia dawa hizi hujikuta wanabeba mapacha.mfano dawa za clomiphene citrate.
kua na watoto tayari;
wanawake ambao wamezaa mtoto mmoja au wawili kabla wana nafasi kubwa sana ya kuzaa mapacha kuliko wale ambao hawajawahi kuzaa kabisa, ukifuatilia mapacha wengi hua hawazaliwi mimba ya kwanza ila kwanzia mimba ya pili kwenda mbele.
kupata mimba ukiwa kwenye dawa za majira;
japokua sio rahisi sana lakini tafiti zinaonyesha kwamba mimba zinazoingia kwa bahati mbaya mwanamke akiwa anatumia dawa za uzazi wa mpango hutengeneza mapacha lakini pia mimba zinazoingia muda mfupi baada ya kuacha dawa za uzazi wa mpango hua zinaleta watoto mapacha.
urefu na unene;
tafiti zinzonyesha kwamba wanawake warefu wana nafasi kubwa sana ya kubeba mimba za mapacha kuliko wanawake wafupi, lakini pia wanawake wanaobeba mimba wakiwa wanene wanakua na nafasi kubwa sana ya kupata mapacha.
chakula;
jamii ambazo chakula chao kikuu ni viazi vikuu, zimeonyesha kua na mapacha wengi kuliko jamii zingine, tafiti zinasema kwamba viazi hivyo vina kiasi kikubwa sana cha homoni za oestrogen ambazo zinasababisha mama kutoa mayai mengi kitaalamu kama hyperovulation.
endelea kunyonyesha mtoto wako kwa muda mrefu;
kuna homoni moja inaitwa prolactin ambayo inahusika na kutoa maziwa kipindi mama ananyonyesha, sasa kuendelea kuwepo kwa homoni hii kwa kiasi kikubwa wakati mama ameanza kushiriki tendo la ndoa kuna muongezea nafasi kubwa ya kupata mapacha akibeba mimba.
matumizi ya dawa za folic acid;
dawa za folic acid hutumika na wajawazito wote ili kuzuia uwezekano wa kuzaa mtoto mwenye matatizo ya kimaumbile hasa kwenye mishipa ya fahamu, lakini matumizi ya dawa hizi mwezi mmoja kabla ya kubeba mimba yanaongeza uwezekano mkubwa wa kubeba mimba za mapacha.
kua pacha mwenyewe; kama wewe mwenyewe ulizaliwa kama mapacha basi uwezekano wa kubeba mimba ya mapacha ni mkubwa sana kuliko wale wengine ambao walizaliwa kawaida.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
5 comments:
Kwa anayehitaji watoto mapacha WA kufanana na kutokufanana..dawa zz ugumba..uzazi..wasiliana na dr tiba asili 0744903557 tanga
Enter your comment...good
Thanks dokta
Hakika nimefurahi na kujifunza mana mm ni pacha natumai kupata pacha pia
Sasa nimekata tamaaa maana hakuna pacha kwenye ukooo wetu hata wakisingiziwa
Post a Comment