Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemshauri msanii wa singeli
Manfongo, kutumia lugha za misamiati na mafumbo katika kazi zake ili
kuepusha maneno ya mtaani ambayo yanatafsirika kwa kuwa muziki huo
unasikilizwa na watu wa rika tofauti.
Manfongo
leo akiwa kwenye kipindi cha ‘Planet Bongo’ cha East Africa Radio
amesema baada ya muziki wa singeli kuonekana kushika kasi sana BASATA
walimtaka kutumia...
misamiati ambayo haijakaa kihuni huku wakitolea mfano
mistari iliyomo kwenye wimbo wa 'Hainaga Ushemeji'.
“Katika wasanii wote wa
singeli peke yangu ndiyo nmejiandikisha BASATA, baada ya kutoka India
kwenye 'Show' wakaniita kwa sababu mimi ndiyo msanii wa singeli mwenye
tuzo, wakanambia sasa Manifongo wewe umeshakuwa msanii mkubwa tafadhali
kwenye hizi nyimbo zenu inabidi ukawe balozi wa kuwashauri wenzako
mtumie maneno ya kiswahili yenye mafumbo, kiswahili mnachotumia kipo
wazi sana kama hainaga ushemeji ndo nini?”. Alieleza Manifongo.
Aidha Manfongo amewaambia watangazaji
wa kipindi hicho Dullah pamoja na Jay R Junior kwa sasa anataka kufanya
yale aliyoagizwa kutoka BASATA kwenye kazi zake nyingine ili aweze
kuwashawishi vijana wanaomtazama kama mfalme wa Singeli waweze kuelewa
maneno gani ya kutumia kwenye muziki huo.
Pia msanii huyo ameweka wazi kuachana na
uongozi wake wa mwanzo ambao umeshindwa kuwekeza kwake ikiwa ni pamoja
na kushindwa kusimamia kazi yake ya Kibaka aliyoitoa siku zilizopita na
kushindwa kufanya vizuri.
0 comments:
Post a Comment