Pages

Subscribe:

Tuesday, March 14, 2017

ISHU YA MADAWA VANESSA MDEE AACHIWA KWA DHAMANA



Baada ya kushikiliwa na polisi kwa takriban siku 4, Vanessa Mdee ameachiwa kwa dhamana Jumatatu hii, Vanessa ambaye alishikiliwa muda mfupi baada ya kurejea kutoka Afrika Kusini ni miongoni mwa mastaa waliotajwa kwenye orodha ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana kuhusishwa na matumizi na biashara ya dawa za kulevya.

Inadaiwa kuwa Vee anatetewa na mwanasheria maarufu, Peter Kibatala.
Watu wengi wakiwemo mastaa nchini walikuwa wakimtetea kutaka kuachiwa huru kutokana na...
kile wanachoamini kuwa anaonewa.

Vanessa Mdee atakiwa kuripoti kituo cha polisi cha kati (Central) Jumatano hii.
Kwa mujibu wa maelezo ambayo Bongo5 imepatiwa kutoka kituoni hapo, hitmaker huyo wa Cash Madame ameachiwa kwa dhamana Jumatatu hii, baada ya kufanyiwa mahojiano ya mwisho hiyo jana.

Mrembo huyo amekuwa akishikiliwa na jeshi la polisi tangu Jumatano iliyopita. Vanessa ni miongoni mwa mastaa waliotajwa kwenye orodha ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana kuhusishwa na matumizi na biashara ya dawa za kulevya.

0 comments:

Post a Comment