Inapotokea wafalme wa Misri, Malkia wa Ulaya, Mitume na wanasayansi wa
kisasa wanakuja na kukubaliana katika jambo moja, ni mhimu kudadisi juu
ya jambo hilo. Ingawa nyakati za sasa tunazungukwa na taarifa na elimu
nyingi kuliko katika wakati mwingine wowote, bado tunahitaji kujifunza
vitu kutokana na historia na maisha ya kale.
Kutoka kwa baba wa sayansi ya matibabu katika nchi za magharibi
Hippocrates kwenda mpaka kwa kiongozi wa mfumo wa mwisho wa kifarao
Cleopatra hadi kwa mfalme Tut na jamii iliyofuata, kitu cha pekee
ambacho... walikuwa wakifanana viongozi hawa kwa pamoja ilikuwa ni thamani
waliyoiona katika mtishamba fulani.
Mtishamba au mmea huo ambao viongozi hao walikutana pamoja si mwingine
bali ni habbat soda. Habbat soda ndilo jina linalotumika zaidi mashariki
ya kati na huko ulaya hujulikana zaidi kama ‘black seeds’.
Kwahiyo niliamua kuchukua muda kusoma na kupeleleza zaidi kuhusu habbat
soda kwa ajili yangu mwenyewe na ya wasomaji wangu ili hatimaye niweze
kukuletea mwanga kamili juu ya mengi yanayosemwa kuhusu mafuta ya
habbat soda.
Unaweza kuwa umesikia majina tofauti tofauti ya habbat soda kutegemea na
sehemu gani ya dunia ulipo. Haya ni moja ya majina yake:
Kalonji Oil
Black Cumin Seed Oil
Nigella Seeds
Graine De Nigelle
Black Onion Seeds
Schwarzkummel
Mafuta ya habbat soda yanatokana na mbegu za habbat soda na mbegu hizi
huwa ni nyeusi na ndiyo maana kwa kiingereza wanaita ‘black seed’. Kuna
mashine nyingi za nyumbani unazoweza kutumia kutengeneza mafuta yako
mwenyewe kutoka katika mbegu za habbat soda ingawa bado nakushauri
ununuwe yale ambayo yameandaliwa tayari.
Habbat soda ina sifa hizi:
Huondoa bakteria mwilini
Huondoa uvimbe
Huondoa sumu mwilini
Inaondoa fangasi
Inatibu kansa
Inatibu pumu
Inadhibiti kazi za histamini
Inaua virusi
Inazuia damu kuganda
Vitu viwili mhimu zaidi ambavyo mafuta haya yanavyo ni ‘thymoquinone’ na ‘thymohydroquinone’.
Vimeng’enya hivi viwili ndivyo vinaweza kusemwa kuwa ndiyo sababu ya
mafuta haya kuwa ni dawa kwa kila ugonjwa. Vinaimarisha moja kwa moja
kinga yako ya mwili na kuifanya ipatikane wakati wowote itakapohitajika
na mwili. Vimeng’enya hivi viwili ndivyo inaaminika ndiyo sababu mfalme
Tut alipatikana na chupa ya mafuta ya habbat soda kwenye kaburi lake
akitumaini kuyachukua na kuyatumia atakapofufuka!
Mtume Muhammad (S.A.W) amewahi kunukuliwa akisema ‘MAFUTA YA HABBAT SODA NI DAWA KWA KILA UGONJWA ISIPOKUWA KIFO’
Mbegu za habbat soda zinatoka katika majani ya mmea ujulikanao kama
‘Nigella Sativa’ na unalimwa karibu katika kila pembe ya dunia kwa sasa.
Asili yake ni Afrika kaskazini, mediterania/ulaya na Asia na kutoka
hapo umesambaa kila sehemu ya dunia. Habbat soda inachukuliwa kama moja
ya dawa za asili bora zaidi kuwahi kutokea.
Nini yanachoweza kufanya mwilini haya mafuta ya habbat soda? kuna
matumizi mengi ya habbat soda katika kutibu na kukinga magonjwa
mbalimbali. Hapa nimejaribu kukusanya baadhi ya magonjwa 90 ambayo
unaweza kujitibu kwa kutumia habbat soda.
Kama kawaida unapewa angalizo kutotumia dawa yoyote bila uangalizi wa karibu wa daktari
Magonjwa 90 yanayoweza kutibika na habbat soda ni pamoja na:
1. Yanaimarisha afya ya moyo
Afya mbovu ya moyo inaweza kuwa ni matokeo ya sababu nyingi lakini
sababu zote chanzo chake kikuu ni matokeo ya kutokuupa moyo virutubishi
unavyovihitaji.
Mafuta ya habbat soda yana asidi mafuta safi na yenye Omega 6 na 9, pia
yana kirutubishi kingine mhimu zaidi kijulikanacho kama “phytosterols”
ambacho husaidia kulazimisha kusinyaa na kutanuka kwa mishipa ya damu na
hivyo kusaidia kuzuia damu kuganda na kujikaza katika ateri. Viinilishe
hivi pia husaidia kushusha lehemu kwenye damu na kiasi cha damu sukari.
Kwa karne nyingi mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika kutibu matatizo mengi yanayohusiana na moyo.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja mpaka miwili
2. Hupigana na maambukizi ya fangasi
Maambukizi ya fangasi yanatokea wakati bakteria wanapozidi juu ya ngozi
yako na kupelekea kutokea kwa magonjwa mengi ikiwemo miwasho, upele na
ukurutu. Tafiti zinaonyesha mafuta ya habbat soda ni mazuri kwa tiba
karibu kwa kila aina ya fangasi kitu kinachopelekea wanasayansi wengi
kuamini kuwa habbat soda ni dawa ya asili na mbadala mhimu zaidi kwa
kila mtu kuwa nayo nyumbani.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda
kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja. Mengine pakaa kama mafuta yako ya kupakaa
sehemu yenye muwasho kutwa mara 3 hadi 3
3. Hudhibiti Aleji (mzio)
Wengi wetu tunapatwa na aleji na kutokewa na chafya au mafua yasiyoisha
na kupelekea kushuka kwa kinga yetu ya mwili. Kutumia mafuta asili ya
habbat soda kwa ajili ya kutibu aleji kunaweza kuleta matokeo mazuri
bila gharama kubwa. Na siyo kwamba mafuta haya yatakupa nafuu kwa haraka
sana dhidi ya aleji tu, bali pia yatakufanya kujisikia nafuu haraka
zaidi kuliko dawa nyingine nyingi za kutibu aleji za viwandani zilizopo
sokoni leo.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja mpaka miwili.
4. Ni mafuta mazuri kwa ajili ya ngozi yako
Iwe ni muonekano au afya ya ngozi kwa ujumla, ipo sababu kwanini watu
wanapenda kuwa na ngozi ya kupendeza na yenye afya. Mafuta ya habbat
soda yana asidi mafuta mhimu zaidi, yana vitamini nyingi, yana viondoa
sumu vya kutosha na asidi amino mhimu ambazo miili yetu huzihitaji.
Mafuta ya habbat soda ni mafuta safi ya ngozi kwa nyakati zote za siku
na kwa siku zote. Mafuta haya pia yanasaidia ngozi kutokuungua moja kwa
moja na miale ya jua huku yakizuia usizeeke haraka kwa kuondoa mikunjo
yoyote kwenye ngozi yako. Matumizi: Yawe ndiyo mafuta yako ya kupakaa
mwilini kila siku
5. Hutibu kansa ya ngozi (Melanoma)
Kansa ni matokeo ya kinasaba cha damu (DNA) kujizidisha au kujizalisha
mara nyingi na kwa haraka zaidi dhidi ya uwezo wa kinga ya mwili. Mara
nyingi kansa hutokeza vivimbe sehemu mbalimbali mwilini. Mafuta ya
habbat soda yana virutubishi vingine viwili ambavyo ni ‘thymoquinone’ na
‘thymohydroquinone’ ambavyo utafiti unaonyesha huwa vina uwezo wa
kudhibiti kansa kwenye ngozi na kansa nyingine mbalimbali mwilini. Hii
ni kutokana na sifa yake ya haya mafuta katika kuzuia uvimbe na
bakteria, sifa kuu mbili za habbat soda.
Habbat soda hufanya hivyo kwa kuzilenga seli zako nyeupe za damu kwa
kuziongezea kinga ya mwili na hivyo kuua seli za kansa. Matumizi: kama
namba 4 hapo juu.
6. Hutibu chunusi
Chunusi ni matokeo ya moja kwa moja ya vivimbe kwenye ngozi hasa ya paji
la uso na usoni kwa ujumla. Mafuta haya yanaondoa uvimbe wa aina yoyote
kwenye ngozi na kuitengeneza upya ngozi huku yakiiacha nyororo na
muonekano wake wa asili. Mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika kwa
ajili hii ya kutunza na kutibu maradhi mbalimbali ya ngozi na wafalme na
malkia wengi katika historia yote ya dunia.
Matumizi: Yawe ndiyo mafuta yako ya kupakaa mwilini kila siku. Unaweza
pia kunywa kijiko kidogo kimoja kila siku kusafisha mwili ndani
7. Hutibu maambukizi
Maambukizi ya aina yote hupigwa na kinga ya mwili hasa na seli nyeupe za
damu ndizo zinazohusika na kazi hiyo. Kwa kuiongezea nguvu kinga ya
mwili moja kwa moja, mafuta ya habbat soda yanausaidia mwili wako
kupigana na maambukizi kutoka kwenye nywele kichani mpaka kwenye kucha.
Hii ni sifa ya pekee ya habbat soda ambayo imekuwa ikijulikana kuwa nayo
katika historia yote ya dunia tangu enzi hata leo bado ni moja ya dawa
za asili zenye nguvu ya kupigana na maambukizi ya aina nyingi ya mwili.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja mpaka miwili
8. Hutibu tatizo la ugumba
Ugumba unaweza kutokea kutokana na sababu nyingine nyingi, ingawa
imethibitishwa pasipo na shaka kwamba mafuta ya habbat soda yamewasaidia
wengi kuimarisha afya zao za uzazi. Kwa wale wote wenye tatizo la uzazi
au ugumba tambueni kuwa mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika
kutibu matatizo ya ugumba kwa zaidi ya miaka 2000 sasa. Mpaka leo bado
mafuta ya habbat soda yanaendelea kuripotiwa kama ndiyo dawa bora zaidi
ya asili kwa ajili ya kurekebisha tatizo la ugumba kwa watu wa jinsia
zote mbili.
Wakati huo huo mafuta ya asili ya habbat soda yamethibitika kuwa dawa
bora zaidi ya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake na hutibu
tatizo la nguvu za kiume hata kama mwanaume utakuwa na umri wa miaka
120. Unachohitaji ni kuyatumia kwa kipindi kirefu hata miezi miwili au
hata zaidi mfululizo kama tatizo limekuwa sugu sana.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1
9. Huotesha nywele
Moja ya matumizi makubwa ya mafuta haya ni kuotesha nywele. Bidhaa
nyingi sokoni zinazotumika kwa ajili ya kuotesha nywele zinaacha madhara
makubwa zaidi kuwa mtumiaji kuliko faida zake. Kwahiyo kwa wale wenye
tatizo la upala, nywele zisizokuwa na kwa wale ambao nywele zao hazina
afya mnashauriwa kuchagua mafuta haya kwa matatizo haya yote. Ingawa
haieleweki ni kwa namna gani mafuta haya yanakuza nywele lakini
wanasayansi wanaamini haya yanaweza kuwa ni matokeo uwezo wake mkubwa wa
kuondoa sumu na protini nyingi ndani yake. Mafuta ya habbat soda kwa
ajili ya nywele yenyewe ni meusi kabisa kabisa na huwa mazito kidogo.
Matumizi: Sugulia kipande cha limao fresh eneo ambalo nywele
zimenyonyoka na kisha pakaa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya habbat
soda ya nywele na uache kama dakika 15 hadi 20, unaweza kuacha hivyo
hivyo au ujisafishe na maji safi, unaweza kufanya kutwa mara 1 au 2 kwa
mwezi mmoja hadi miwili
10. Hutibu mafua na homa
Mafua na homa ni matokeo ya kushuka kwa kinga ya mwili na kadri
unavyoendelea kuyavumilia magonjwa kama haya ndivyo unavyozidi
kuidhoofisha zaidi kinga yako ya mwili. Kama tulivyoona kabla kuwa
mafuta ya habbat soda huongeza kwa haraka sana kinga ya mwili, huondoa
haraka sumu mwilini na bakteria mbalimbali na hivyo kufanya kuwa ndiyo
dawa nzuri ya asili dhidi ya mafua na homa za mara kwa mara.
Chukua kijiko kikubwa kimoja cha mafuta haya na vijiko vitatu vikubwa
vya asali changanya katika glasi moja (ml 250) ya maji ya uvuguvugu na
unywe kutwa mara moja kila siku. Kitendo hiki hakitakuondolea mafua na
homa pekee bali pia kitaimarisha afya yako kwa ujumla. Fanya kwa siku 7
hadi 14
11. Hutibu majipu
Liwe ni jipu moja au majipu mengi kwa pamoja, mafuta ya habbat soda
ndiyo dawa nzuri kukupatia nafuu ya haraka. Hii ni kwa sababu kwa sehemu
kubwa majipu ni matokeo ya maambukizi ya bakteria na mchafuko wa damu.
Na mafuta ya habbat soda ni wakala mzuri wa kuondoa bakteria na
kusafisha damu na hivyo kuwezesha majipu kuwa chini ya ulinzi.
Unaweza kupakaa mafuta haya juu ya jipu moja kwa moja na wakati huo huo
mengine unywe kama ilivyoelezwa kwenye namba 9 hapo juu. Hata hivyo
ikiwa jipu ni kubwa sana na huoni nafuu hata baada ya kujaribu mafuta
haya muone daktari kwa msaada zaidi.
12. Hutibu kikohozi na Pumu
Ile sifa yake kuu ya kuondoa vivimbe kwenye tyubu za koo, kitendo chake
cha kuongeza kinga ya mwili, kuua bakteria na virusi ndiyo sababu za
mafuta haya kutumika kutibu kikohozi na pumu.
Imeandikwa katika historia kuwa mababu wa zamani wa Misri walikuwa
wakitumia mafuta ya habbat soda hasa kwa ajili ya kuimarisha afya ya
mfumo mzima wa upumuwaji.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kwa wiki 3 hadi 4 hivi
13. Hutibu kuharisha
Mara nyingi kuharisha ni matokeo ya maambukizi ya virusi na bakteria na
kama tulivyoona mafuta ya habbat hudhibiti baktria na virusi mbalimbali
mwilini na hivyo kufanya ndiyo dawa nzuri mbadala kwa ajili ya kutibu au
kuzuia kuharisha. Huweka sawa mfumo wa umeng’enyaji wa chakula na tumbo
kwa ujumla na hivyo kuzuia mwili wako kupatwa na tatizo la kufunga
choo. Inashauriwa kuchanganya kijiko kidogo kimoja cha chai au viwili
vya mafuta ya habbat soda na kikombe kimoja cha mtindi na utumie asubuhi
na usiku kwa siku mbili hivi na kuharisha kutasimama.
14. Hutibu shinikizo la juu la damu
Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya shinikizo la juu la damu ni moja kati
ya matumizi makubwa ya mafuta haya kwa sasa. Ingawa haijathibitishwa
rasmi kama dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu lakini wagonjwa wengi
wa shinikizo la juu la damu wameripoti kushuka kwa kiwango kikubwa cha
mashinikizo yao ya damu wakati wanapotumia mafuta haya ya habbat soda.
Tafiti kama hizi => http://goo.gl/VOSJp4 zimepelekea wengi kuanza
kutumia mafuta ya habbat soda kama dawa ya asili kwa ajili kutibu
shinikizo la juu la damu.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda
kutwa mara 1 kwa wiki 3 hadi mwezi mmoja. Pia hakikisha unakuwa na
uzito sawa kulingana na urefu wako. BP ya juu inaweza kuchelewa kupona
ikiwa uzito wako upo juu ya inavyotakiwa uwe nao.
15. Huondoa tatizo la kukosa usingizi
Tafiti zinaonyesha mafuta ya habbat soda ni dawa nzuri ya asili dhidi ya
tatizo la kukosa usingizi na matatizo mengine kama hayo ya kuvuruga
utulivu wa usingizi kwa ujumla. Watu wengi wameripoti kupata usingizi
mororo na utulivu kwa ujumla kwa kutumia habbat soda.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa.
16. Huzuia mishtuko na kukakamaa kwa mishipa
Mafuta ya habbat soda ni dawa nzuri ya kuzuia kukakamaa na mishtuko
mbalimbali kwenye mishipa. Unaweza kuyanywa mdomoni au unaweza kupakaa
na kuchua moja kwa moja sehemu ya mishipa yenye matatizo kwa ajili ya
matokeo mazuri ya haraka.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
kwa majuma kadhaa. Pakaa pia sehemu ya mishipa yenye matatizo
17. Huondoa kichefuchefu na mvurugiko wa tumbo
Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya kuondoa kichefuchefu na kuvurugika wa tumbo ni moja ya sifa nyingine kubwa ya mafuta haya.
Uwezo wa mafuta haya kutibu haya matatizo mawili unatokana na nguvu yake
kuhamasisha vimeng’enya vyakula vya mwili wako na kuondoa gesi tumboni.
Matumizi: Kwa ajili ya kuondoa kichefuchefu changanya kijiko kidogo
kimoja cha mafuta ya habbat soda na glasi moja ya juisi ya tangawizi na
unywe glasi moja asubuhi na nyingine jioni kila siku kwa siku mbili
tatu.
18. Dawa bora kwa matatizo ya meno
Dawa nyingine nzuri kwa matatizo ya meno kama jino kuuma, kuoza,
kutoboka, kulegea nk ni mafuta ya asili ya habbat soda. Kuondoa maumivu
ya jino unachohitaji kufanya ni kunyunyiza matone kadhaa ya mafuta haya
juu ya hilo jino na utulie tuli kama dakika mbili hivi kutwa mara mbili.
19. Huua seli za kansa ya damu
Tafiti zinaonyesha mafuta ya habbat soda yanacho kitu mhimu sana
kiitwacho kwa kitaalamu kama “thymoquinone” ambacho huziua seli za kansa
ya damu (leukemia HL-60 cells).
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa
20. Hutibu saratani ya matiti
Mafuta ya habbat soda yana uwezo wa kuzuia seli za saratani ya titi
kuendelea kujizalisha na inashauriwa kwa ajili ya kutibu saratani ya
titi yatumike kwa kipindi kirefu miezi hata miwili au zaidi.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
21. Hutibu saratani ya utumbo mpana
Kimeng’enya kiitwacho ‘thymoquinone’ kilichomo kwenye mafuta ya habbat
soda na sifa yake kubwa ya kuondoa sumu ndivyo vitu viwili
vinavyoyawezesha mafuta ya habbat soda kuzishambulia na kuziua seli za
saratani ya utumbo mpana (colon cancer). Yanabaki kuwa ndiyo dawa
mbadala bora zaidi kwa saratani ya utumbo mpana inayosumbua watu wengi
miaka ya karibuni.
Habbat soda si dawa ya magonjwa mengine mengi tu bali pia ni moja ya
vitu mhimu sana katika kuzuia kukua, kujizidisha au kujizalisha upya kwa
seli mbalimbali za kansa.
Uwezo wa mafuta ya habbat soda kudhibiti uongezekaji wa seli za kansa
unashawishi sana kiasi kwamba madaktari wengi wamekiri kuwa ni dawa moja
bora sana mbadala dhidi ya saratani ya kwenye utumbo mpana.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku mpaka upone
22. Hutibu fangasi ya ngozi na mapunye
Fangasi, mapunye, ukurutu na magonjwa mengi ya ngozi yanaweza kutibika
kwa kutumia mafuta ya habbat soda. Fangasi na mapunye ni tatizo
linalowapata watu wengi karibu kila sehemu katika nchi tajiri hata
katika nchi maskini pia.
Unaweza kuyanywa mdomoni na wakati huo huo ukapaka moja kwa moja juu ya
ngozi sehemu yenye tatizo kwa majuma kadhaa. Kama ni kunywa basi kunywa
kijiko kidogo kimoja cha chai kila siku mpaka upone
23. Husaidia kupunguza uzito
Uwezo wa mafuta ya habbat soda kushusha uzito unatokana na sifa yake ya
kuweza kupunguza sukari katika damu. Zaidi ya kuwa ni wakala muondoa
sumu mwilini wa asili, mafuta ya habbat soda husaidia pia kuongeza nguvu
katika mfumo wa umeng’enyaji wa chakula na kupunguza kiasi chako cha
njaa. Hii ya kudhibiti kiasi cha njaa ni mhimu sana hasa wakati unataka
kudhibiti mfumo wa vyakula unavyokula.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
kwa majuma kadhaa, usisahau pia kufanya mazoezi ya kukimbia (jogging
kila siku)
24. Hutibu Kisukari
Kitu gani kimeyafanya mafuta ya habbat soda kuwa ndiyo dawa nzuri ya
asili dhidi ya Kisukari? Ni ule uwezo wake mkubwa wa kushusha shinikizo
la damu na kusaidia wagonjwa wa Kisukari wote ambao ni tegemezi au si
wategemezi wa insulin. Ni dawa nzuri kwa watu wote wenye kisukari aina
ya kwanza na Kisukari aina ya pili kwa wakati mmoja. Pia huboresha kwa
ujumla AFYA ya damu yako.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 2 kila siku kwa mwezi mmoja hadi miwili
25. Hutibu kifafa na mishtuko ya moyo
Dawa nyingi za kisasa zinazotumika kutibu kifafa na mishtuko ya moyo
huwa zina orodha ndefu ya madhara mabaya (negative side effects) pia.
Bahati nzuri kwa upande wako wewe unayesoma makala hii ni kuwa mafuta ya
asili ya habbat soda (black seed oil) ni dawa nzuri ya kutuliza kifafa
na matokeo yaletwayo na kifafa.
Baadhi ya tafiti zimeonyesha watu wenye kifafa na mishtuko ya moyo
waliacha kuonyesha tabia au dalili za kifafa au mishtuko ya moyo
walipotumia mafuta ya habbat soda kwa wiki 4 hadi 6 huku wakitumia
sambamba na dawa walizopewa hospitalini. Watafiti wengi wanasema hii ni
kutokana na kiinilishe mhimu kilichomo kwenye mafuta haya
kijulikananacho kama ‘thymoquinione’. Kunywa kijiko kidogo kimoja cha
chai kutwa mara 1 kila siku mpaka upone.
26. Hutibu vidonda vya kooni
Mafuta ya habbat soda yamethibitishwa kutibu vidonda vya kooni (tonsils)
na kuondoa kila aina ya maumivu kooni na kuondoa uhitaji wa dawa za
kuondoa maumivu (pain killers).
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa
27. Hutibu kidonda ndugu (MRSA)
Kidonda ndugu au kama kinavyojulikana kwa kitaalamu kama ‘Methicillin
resistant Staphylococcus aureus (MSRA)’ ni ugonjwa unaoendelea
kuwasumbua wataalamu wengi katika mahospitali maeneo mengi duniani. Mara
nyingi hutokea kama matokeo ya kudhoofika kwa kinga ya mwili. Uwezo wa
kuondoa uvimbe na sumu wa mafuta haya unayafanya kuwa dawa mbadala yenye
ufanisi zaidi katika kutibu kidonda ndugu.
Mafuta ya habbat soda yatakusaidia kutibu kidonda cha aina hii bila
shida yoyote, yatazuia pia kuendelea kuongezeka au ksambaa zaidi kwa
kidonda hiki.
Kama kuna matumizi mhimu sana ya dawa hii basi ni hili la kutibu vidonda
mbalimbali ikiwemo kidonda ndugu kidonda ambacho huletwa na bakteria na
kuwa sugu kutibika kwa dawa nyingi za kawaida.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
kwa majuma kadhaa pia pakaa haya mafuta hasa yale ya grade 1 kwenye
kidonda kutwa mara 1
28. Huondoa utegemezi wa madawa ya kulevya
Kutumia mafuta ya habbat soda kuondoa utegemezi (uteja) kwa madawa ya
kulevya na vilevi vingine ni moja ya kazi nyingine zilizothibitika
kufanywa na mafuta haya.
Katika majaribio, mafuta ya habbat soda yameonyesha kuwa msaada mkubwa
kutuliza hali ya kujisikia vibaya na mauzauza mengine yatokanayo na
kuacha kutumia dawa za kulevya na wakati huo huo yameonyesha kudhibiti
hamu ya kutaka kurudia tena matumizi ya madawa ya kulevya baada ya mtu
kuamua kuacha.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa mwezi mmoja na nusu mpaka miwili
29. Huondoa makovu
Iwe ni makovu ya upasuaji uliopita au ni makovu mengine yoyote, mafuta
ya habbat soda ndiyo dawa nzuri kwa ajili ya kuondoa makovu. Ni moja
kati ya dawa mbadala chache ambazo zimethibitishwa kuondoa na kutibu
makovu moja kwa moja.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa hasa habbat soda grade 1
30. Hutibu kansa ya mlango wa kizazi
Kansa nyingine ambayo mafuta ya habbat soda yamethibitika kuitibu ni
kansa ya mlango wa kizazi (cervical cancer). Hii tena inawezekana
kutokana na kimeng’enya ‘thymoquinione’ kipatikanacho kwenye haya
mafuta, tafiti zinaonyesha kuwa husaidia pia kwa kuziongezea nguvu na
idadi seli nyeupe za damu na kuzidhibiti seli za kansa kuendelea
kujizalisha.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa hasa habbat soda grade 1
31. Huzuia madhara ya miale ya jua
Tafiti zinaonyesha kuwa watu waliokuwa wakitumia mafuta ya habbat soda
na kukaa kwenye jua masaa mengi walipatwa na madhara machache ya miale
ya jua kulingalisha na wale ambao walikaa juani muda mrefu bila kutumia
habbat soda.
Kiasi kikubwa cha kinga ya mwili kilionekana kwa watu waliokuwa
wakitumia mafuta ya habbat soda. Kuna tafiti pia zinazothibitisha habbat
soda kuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa wa kansa walio kwenye matibabu ya
mionzi.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda
kutwa mara 1 kila siku, pia pakaa kama mafuta yako ya kupakaa kwenye
ngozi kila siku
32. Huzuia na kutibu athari za sumu ya risasi
Sumu ya risasi (lead) ndiyo moja ya sumu zinazowapata watu wengi dunia
nzima sababu ya maendeleo ya viwanda na matumizi ya madawa ya
mashambani. Risasi inaweza kuleta shida na mambo mengi kuhusiana na kazi
za mwili wako kwa ujumla na kuleta matatizo katika moyo, tumbo, figo,
mfumo wa fahamu, mifupa na hata katika mfumo wako wa uzai.
Tafiti zimeonyesha kwamba mafuta ya habbat soda kuwa na uwezo mkubwa
kuzuia na kurekebisha madhara katika ubongo yaliyotokana na sumu ya
risasi.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda
kutwa mara 1 kila siku, pia pakaa kichwani kila siku yale ya nywele
nayo yamethibitika kuwa yanatibu maumivu ya kichwa na matatizo mengine
mengi kuhusiana na kichwa
33. Huimarisha ukuwaji wa ndevu
Tafiti zimeonyesha mafuta ya habbat soda yanaweza kuhamasisha ubora na
ukuwaji wa ndevu kidevuni. Ingawa hii siyo kazi yake hasa ya msingi,
unaweza kupakaa moja kwa moja mafuta ya habbat soda ya nywele juu ya
kidevu chako na utaona ndevu zinakuwa na afya nzuri, zinakuwa haraka na
kuziacha zenye unyevunyevu pia.
34. Hutibu maumivu ya kuumwa na nyuki na nyigu
Unga wa habbat soda ukichanganywa na maji kidogo ni dawa nzuri kabisa ya
asili kwa maumivu au uvimbe kutokana na kuumwa na wadudu kama nyigu na
nyuki. Chua sehemu iliyoathiriwa na mchanganyiko huu kutwa mara mbili
kwa siku 2 au 4 hivi.
35. Huondoa msongamano kifuani
Mwagia na uchue kwa dakika kadhaa juu ya kifua chako na mafuta ya habbat
soda kuondoa msongamano (makohozi, gesi nk) kifuani. Utapata matokeo
mazuri zaidi kama utachanganya mafuta haya na asali kwa ajili ya hili
zoezi. Unaweza pia kuamua kunywa mdomoni kijiko kidogo kimoja cha chai
kila siku badala ya kupaka juu ya kifua.
36. Hutibu maumivu ya sikio
Mafuta ya habbat soda yakichanganywa na mafuta ya zeituni yanaweza
kutibu maumivu ya sikio na miwasho mingine masikioni. Changanya nusu
kijiko kidogo cha mafuta ya habbat soda na nusu kijiko kidogo kingine
cha mafuta ya zeituni, pasha moto kidogo mchanganyiko huu na kuweka
matone mawili matatu sikioni sehemu iliyoathirika.
Unaweza kuweka skafu au kofia juu ya sikio dakika 2 baada ya kunyunyiza
matone ya mchanganyiko huu na utulie sehemu moja kwa dakika kadhaa.
37. Dawa nzuri ya magonjwa ya macho na kuona
Mafuta ya habbat soda yanaweza kutumika pia kutibu maambukizi ya kwenye
macho na wakati huo huo kuongeza uwezo wa macho kuona (eyesight and
vision). Yametumika pia na watu wengi kutibu maambukizi ya kwenye macho
yao ambayo hupelekea macho kuwa mekundu.
Ili kutibu hayo unaweza pakaa mafuta haya sehemu zinazozunguka jicho
lako kabla ya kwenda kulala na unaweza kufanya zoezi hili kila siku kwa
matokeo ya haraka zaidi.
38. Hutibu kiharusi
Unapougua kiharusi hasa usoni, mafuta ya habbat soda yanaweza kuleta
nafuu haraka. Weka kiasi cha mafuta ya habbat soda kwenye bakuli au
sahani na usogeze pua yako karibu na mafuta na unuse nuse mafuta hayo.
Chukua sekunde 10 mpaka 20 kuvuta pumzi ndani kwa nguvu na urudie zoezi.
Fanya zoezi hili kila siku mpaka upone.
39. Huondoa msongamano puani
Habbat soda pia hutumika kuzibua na kuondoa msongamano puani. Hii ni
moja ya kazi ambayo mafuta haya yanazifanya vizuri zaidi. Unaweza
kuyanywa na wakati huo huo kuyanusa puani kama nilivyoeleza kwenye namba
38 hapo juu.
40. Huondoa mawe kwenye kibofu cha mkojo
Kutumia mafuta ya habbat soda kwa ajili ya kuondoa mawe kwenye kibofu
cha mkojo ni njia nzuri ya kuondoa maumivu na mawe katika kibofu cha
mkojo kwa pamoja. Uwezo mkubwa ulionayo mafuta haya katika kuondoa
vivimbe na sifa yake ya kuondoa sumu ndivyo vitu vinavyoyafanya mafuta
haya kuwa dawa bora ya asili ya kuondoa mawe katika kibofu cha mkojo.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kila siku mpaka upone.
41. Huondoa mawe katika Ini
Kama ilivyo kwa mawe katika kibofu cha mkojo, mawe katika ini pia
yanaweza kusababisha maumivu na madhara mengine makubwa wakati ukijitibu
kwa kutumia dawa za viwandani. Sifa za mafuta ya habbat soda huondoa
mawe katika ini kwa hali ya mwendelezo mpaka yatakapoondoka yote. Kunywa
mafuta haya yakichanganywa na asali kwa matokeo mazuri zaidi. Kijiko
kidogo kimoja unaongeza na asali kijiko kidogo kimoja. Tumia kwa mwezi
mmoja hivi
42. Huondoa gesi tumboni
Mafuta ya habbat soda huusaidia mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula na
hivyo kukusaidia kuondoa gesi. Pia yamethibitika kuondoa mvurugiko wa
tumbo na takataka nyingine tumboni kwa haraka zaidi.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kila siku mpaka upone kabisa
43. Hutibu bawasiri
Dawa nyingi zinazotumika kutibu bawasiri zina madhara mengine mabaya na
nyingi ya hizo hazitibu kabisa bawasiri na kulazimisha wengine kufanya
upasuaji. Mafuta ya habbat soda kwa upande wake yanatoa suluhu ya haraka
katika kutibu bawasiri na tafiti zinaonyesha yanao uwezo wa kuzuia
kusambaa au kuongezeka kwa ugonjwa huu.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda
kutwa mara 1 kila siku hasa habbat soda grade 1, pia pakaa sehemu yenye
tatizo nje na ndani kutwa mara 2 kwa majuma kadhaa
44. Huondoa maumivu ya kichwa
Faida nyingine mhimu ya mafuta ya habbat soda ni uwezo wake katika
kutibu maumivu ya kichwa na kipanda uso. Kwa karne nyingi Waarabu na
Wazungu wamekuwa wakitumia mafuta haya kwa kupaka maeneo ya karibu na
pua, macho na sehemu ya mbele ya kichwa ili kuondoa maumivu ya kichwa.
Hata ukiyanywa kijiko kidogo kimoja kila siku maumivu ya kichwa
yatapotea.
Pia yale meusi kwa ajili ya nywele nayo yanaondoa maumivu ya kichwa na
hili nimelishuhudia mimi mwenyewe nilikuwa na tatizo la kuumwa kichwa
mara kwa mara sababu ya kukaa kwenye computer masaa mengi lakini tangu
nianze kutumia mafuta haya sijawahi kuumwa kichwa tena.
45. Huongeza kinga ya mwili
Unaweza kutumia mafuta ya habbat soda kuimarisha kinga yako ya mwili kwa
ujumla na hivyo kuongeza ulinzi wa mwili wako dhidi ya magonjwa
mbalimbali ikiwemo dhidi ya bakteria na virusi. Mafuta ya habbat soda
ndiyo bidhaa pekee ya asili iwezayo kuimarisha kinga yako ya mwili kwa
muda mfupi.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda
kutwa mara 1 kila siku mpaka kinga yako imeimarika. Unaweza kutumia pia
mafuta haya hata kama huumwi chochote.
46. Husaidia mama anayenyonyesha
Mafuta ya habbat soda yakitumika na mama anayenyonyesha husaidia
kuongezeka kwa uzalishwaji wa maziwa. Kunywa kijiko kidogo kimoja cha
chai kutwa mara 1 kila siku.
47. Huongeza kumbukumbu
Utafiti unaonyesha kuwa mafuta ya habbat soda yana uwezo wa kuongeza
uwezo wako wa kumbukumbu, ufahamu na umakini. Karibuni imethibitika
habbat soda yanaweza kuongeza uwezo wa kukumbuka vitu kwa haraka
vikiwemo vya muda mfupi hata vile vya muda mrefu.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda
kutwa mara 1 kila siku mpaka hali yako ya kukumbuka vitu imekaa sawa.
48. Huondoa madoa meusi kwenye ngozi
Moja ya kazi za mafuta ya habbat soda ambazo wengi hawazijuwi ni hii ya
kuondoa madoadoa au mabaka meusi juu ya ngozi. Unachohitaji ni kuyatumia
kama mafuta yako ya kupakaa kila siku na hutachelewa kuona matokeo.
49. Huondoa maumivu ya kung’atwa na wadudu
Wadudu kama mbu na wengine wanapokuuma huacha pia maumivu fulani na hata
uvimbe. Kupaka mafuta haya juu ya eneo lililoathirika kutasaidia
kuondoa maumivu na uvimbe au muwasho wowote sababu ya wadudu hao.
50. Hutibu kukauka kwa midomo (Lips)
Tatizo hili la midomo ya nje (lips) kukauka limepelekea kutengenezwa kwa
bidhaa nyingi za viwandani kwa ajili hiyo na wanawake ndiyo wanaonekana
kuzitumia zaidi huku baadhi ya bidhaa hizo zikiripotiwa kusababisha
baadhi ya saratani.
Mafuta mhimu (essential oils) yapatikanayo katika mafuta ya habbat soda
yanaweza kuzuia kukauka kwa mdomo na kuzalisha upya ngozi kwenye sehemu
za nje ya mdomo (lips) na kukuachia rangi safi ya asili ya lips zako
bila madhara yoyote mabaya hapo baadaye.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda
kutwa mara 1 kila siku, pia pakaa sehemu ya lips zako kila siku.
51. Yanatibu kufunga choo
Kama vile yanavyokusaidia katika mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula
ndivyo yanavyokusaidia pia kwa tatizo la kufunga choo au kupata choo
kigumu sana. Kuna watu wengine asipopata choo hata siku mbili haoni kama
ni tatizo kwake na mwingine amezoea kupata choo kigumu kila siku na
anaona ni kawaida tu.
Kufunga choo au kupata choo kigumu sana kila mara ni ishara mbaya kuhusu
afya yako. Ni dalili ya moja kwa moja kuwa huna maji ya kutosha mwilini
au maji unayokunywa hayabaki mwilini na yanapitiliza kwenda nje bila
kutumika na mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula.
Mafuta ya habbat soda yanatibu tatizo la kufunga choo (constipation)
bila shida yoyote. Kunywa kijiko kidogo kimoja cha mafuta haya kila
baada ya chakula cha mchana na baada ya chakula cha usiku kwa matokeo ya
haraka.
52. Hutibu maumivu ya mgongo na mishipa
Unaweza kupunguza mahitaji ya dawa za kuondoa maumivu ya mgongo na
mishipa kwa kupaka au kujichua na mafuta ya habbat soda sehemu yenye
maumivu moja kwa moja. Hutakawia kuona nafuu kwa haraka.
53. Husaidia kuondoa maumivu ya tumbo
Kwa matatizo mengi ya tumbo, mafuta ya habbat soda yanaweza kuwa msaada
mkubwa wa kukupa nafuu kwa haraka. Kuondoa maumivu ya tumbo ni moja ya
kazi kubwa inayotambulika na wengi ya mafuta ya habbat soda. Kunywa
kijiko kidogo kimoja kila siku baada ya kula chakula kwa matokeo ya
haraka.
54. Huondoa maambukizi kwenye fizi
Maumivu na maambukizi kwenye fizi za meno vinaweza kuondolewa kwa
kutumia mafuta ya habbat soda. Uwezo wake wa kuondoa sumu na uvimbe
ndiyo sababu ya madaktari wengi kupendekeza itumike kutibu maambukizi
kwenye fizi. Unaweza kutumia kama dawa yako ya mswaki pia uyanywe kijiko
kidogo kimoja kila siku.
55. Hutibu U.T.I
Maambukizi na matatizo mengi kwenye kibofu cha mkojo na njia ya mkojo
kwa ujumla yanatibika na mafuta ya habbat soda ikiwemo ugonjwa wa U.T.I
unaowasumbua watu wengi miaka ya karibuni.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa hasa habbat soda grade 1
56. Huzuia mdomo kukauka
Kutibu tatizo la mdomo kukauka chukua kijiko kidogo kimoja cha mafuta
haya na weka mdomoni kwa sekunde 30 hivi. Jigeuzegeuze kichwa na mdomo
kuhakikisha mafuta yanagusa kila sehemu za mdomo wako kabla ya kutema au
unaweza hata kuyameza. Kisha safisha mdomo na kinywaji kingine kitamu
kama juisi hivi au asali kuondoa radha yake ya ukakasi.
57. Huzuia pua kuvuja damu
Haya ni moja ya matumizi ya asili ya mafuta ya habbat soda nyakati za
joto katika majira ya kiangazi katika jamii nyingi mashariki ya kati.
Kama unapata tatizo la pua kuvuja damu unachotakiwa kufanya ni kuweka
matone mawili au matatu ya mafuta haya ndani ya pua zako na ukae utulie
uone kazi ya mafuta ya habbat soda kuzuia damu kuvuja puani.
58. Huondoa majeraha ya kuungua moto
Kupaka mafuta ya habbat soda juu ya majeraha ya kuungua kwa moto au maji
ya moto kumethibitika kuponya majeraha hayo na kuzalisha upya ngozi.
Kuondoa majeraha hayo chua eneo lenye athari ukitumia mafuta ya asili ya
habbat soda kwa kuondoa maumivu haraka na kuizalisha upya ngozi yako.
59. Hutibu mba kichwani
Mafuta haya si mazuri kwa ajili ya kukuza au kuotesha nywele zako tu,
bali pia huhamasisha ukuwaji wa vinyweleo vya ngozi na hata kuzuia na
kutibu mba. Unachohitaji kufanya ni kupaka mafuta ya kutosha ya habbat
soda kichwani kwako na uache kama dakika 30 hadi 60 hivi na unaweza
kujisafisha au kuacha hivi mpaka utakapoenda kuoga tena.
Na mafuta haya unapoweka kichwani yanadondoka kidogo kidogo hadi kwenye
ubongo na utaona vitu kama maumivu ya kichwa vinaanza kuisha taratibu.
60. Huondoa maumivu kwenye maungio
Moja ya matumizi yanayojulikana na wengi zaidi ya mafuta ya habbat soda
ni kutibu maumivu ya kwenye maungio (joints) mbalimbali mwilini. Utapata
nafuu ya haraka ukitumia mafuta haya kuondoa maumivu katika maungio.
Unaweza kujichua ukitumia mafuta haya moja kwa moja sehemu yenye maumivu
kwa matokeo ya haraka zaidi. Pia kunywa kijiko kidogo kimoja kila siku
kwa matokeo mazuri zaidi.
61. Huzuia kudhurika kwa figo kama matokeo ya Kisukari
Ukiacha ukweli kwamba mafuta ya habbat soda ni dawa mbadala nzuri kabisa
ya kutibu Shinikizo la juu la damu na Kisukari pia ni dawa ya kuzuia
kudhurika kwa figo kama matokeo ya kuugua ugonjwa wa kisukari.
Sababu ya hili ni kutokana na viinilishe mhimu sana vilivyomo kwenye
habbat soda ambayo hujulikana pia kama ‘nigella sativa’ au ‘black
seeds’.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
62. Huweka sawa mzunguko wa hedhi
Mafuta haya yana kazi mhimu sana linalopokuja suala la kulinda na kutibu
matatizo mbalimbali ya uzazi. Matatizo karibu yote ya uzazi kama
maumivu ya tumbo chini ya kitovu, siku za mwezi zisizoeleweka au
kutokuwa na mzunguko maalumu, kukosa hedhi, matatizo katika mfuko wa
uzazi na hata maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Ni dawa nzuri kutumika hata kwa wamama wakubwa wanaopatwa na matatizo
kutokana na kusimama kuona siku zao. Unaweza kuyanywa kijiko kidogo
kimoja kila siku na hata kupaka ndani ya uke mara kwa mara kwani
hutumika pia kutibu .U.T.I na fangasi za ukeni.
63. Mazuri wakati wa ujauzito
Inasisitizwa kuwasiliana na daktari wako wakati wa ujauzito kabla ya
kuamua kutumia dawa yoyote. Hata hivyo mafuta ya habbat soda yameonyesha
matokeo chanya hata yakitumika wakati wa ujauzito ingawa bado hakuna
hitimisho la jumla ikiwa yatumike kwa mama mjamzito au yasitumike sababu
katika baadhi ya kesi yanaonyesha kupunguza kukazika kirahisi kwa
misuli ya mfuko wa nyumba ya uzazi.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
64. Hutibu baridi yabisi (Arthritis)
Mafuta ya habbat soda yamethibitika kuwa dawa bora dhidi ya ugonjwa wa
baridi yabisi, maumivu kwenye mishipa na hali ya mwili kuwaka moto kwa
ujumla.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku mpaka upone.
65. Hutibu vidonda vya tumbo
Ni moja ya dawa za asili chache zinazoweza kutibu vidonda vya tumbo moja
kwa moja. Tafiti nyingi zinathibitisha mafuta ya habbat soda yanatibu
aina zote za vidonda vya tumbo!
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
kwa majuma kadhaa hadi siku 60 hasa habbat soda grade 1. Vidonda vya
tumbo pia upate unga wa asili wa majani ya mlonge na mbegu za maboga kwa
matokeo mazuri na ya uhakika, kumbuka pia kunywa maji mengi ya kutosha
kila siku, epuka pia vinywaji na vyakula vyenye asidi nyingi.
66. Yanaondoa maumivu mbalimbali
Mafuta ya habbat soda yanaondoa mahitaji yako kwa dawa nyingi za kuondoa
maumivu (painkillers) mbalimbali mwilini. Katika kesi nyingi mafuta ya
habbat soda yanaweza kuondoa kabisa mahitaji ya dawa za kuondoa maumivu.
Uwezo wake wa kuondoa vivimbe unayafanya kuwa chaguo zuri zaidi katika
kutibu maumivu yote ya mwili wako kutoka kwenye nywele mpaka kwenye
kucha.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa hasa habbat soda grade 1
67. Hutibu kansa ya Ubongo
Mafuta ya habbat soda ni msaada mkubwa katika kudhibiti na
kusambaratisha vivimbe kwenye ubongo na seli za kansa kwenye ubongo
wako. Makundi kadhaa ya watafiti wamehitimisha kuwa mafuta ya habbat
soda ni dawa halali ya asili kwa ajili ya kutibu kansa ya ubongo na
uvimbe katika ubongo.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
kwa majuma kadhaa hasa habbat soda grade 1. Pia pakaa kichwani moja kwa
moja ama mafuta ya habbat soda ya kawaida au hata yale ya nywele kila
siku.
68. Yanapunguza wasiwasi (Anxiety)
Tafiti zimeonyesha mafuta ya habbat soda kuwa msaada mkubwa katika
kudhibiti tabia za kuhamaki na wasiwasi na hivyo kukuwezesha kujisikia
vizuri kila mara. Na utaona matokeo haya baada ya matumizi ya habbat
soda kwa siku 30 hivi.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku 1
69. Huondoa huzuni na mfadhaiko/stress
Tafiti kadhaa zimeonyesha watu waliokuwa wakitumia mafuta ya habbat soda
wanakuwa ni watu wenye furaha ya asili na kuwa si wepesi kuwa na huzuni
au kufadhaika. Kazi hii ya mafuta ya habbat soda ndiyo mhimu kuliko
zote sababu mamilioni ya watu wanakabiliwa na tatizo la kuwa na
huzuni/stress na mifadhaiko ya akili kitendo ambacho kinaweza kuharibu
kinga zao za mwili na maisha kwa ujumla.
Ni vigumu sana kupata mtishamba ambao unaweza kutibu matatizo
yanayohusiana na saikolojia moja kwa moja lakini mafuta ya habbat soda
yanaweza kutumika kwa dhumuni hili la kutuliza, kupunguza na kutibu
tatizo la huzuni au kufadhaika kwa akili.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
hasa habbat soda grade 1 na kwa matokeo mazuri pata pia mbegu za maboga
zilizokaangwa kidogo na chumvi ya mawe ya baharini na utafune kiganja
kimoja cha mkono wako kila siku mpaka upone, tumia muda mrefu hata miezi
miwili hata zaidi ikibidi.
70. Hutibu kizunguzungu
Historia nyingine katika matumizi ya mafuta ya habbat soda ni katika
kutibu kizunguzungu. Mafuta ya habbat soda yanatambulika kwa kutibu
kizunguzungu na kile unachotakiwa kufanya ni kujichua shingoni na
mashavuni kwa kutumia mafuta ya habbat soda na dalili za kizunguzungu
zinatakiwa zianze kupotea mara moja. Fanya zoezi hili kwa wiki 2 hivi
71. Hutibu Kiungulia
Faida nyigine kubwa ya mafuta ya habbat soda ni kuwa ni dawa ya asili
dhidi ya kiungulia. Ingawa kuna tafiti chache zinazoweza kuthibitisha
hili, bado historia inaonyesha mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika
kutibu kiungulia kwa karne nyingi.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa
72. Huzuia na kutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu
Kumekuwa na tafiti nyingi hivi karibuni ambazo zimeonyesha mafuta ya
habbat soda kuwa msaada mkubwa kwa kuzuia na kupunguza kuongezeka kwa
dalili za ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer). Matokeo
yalionyesha kwamba yakitumika kila siku kijiko kidogo kimoja hadi viwili
vya chai huleta matokeo mazuri zaidi.
73. Hutibu homa ya uti wa mgongo
Nguvu za mtishamba huu zimethibitika kuwa msaada mkubwa katika kutibu
homa ya uti wa mgongo (meningitis). Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa
mafuta ya habbat soda ni moja ya tiba asili nzuri zaidi kwa ajili ya
homa ya uti wa mgongo inayoaminiwa hadi sasa. Kunywa kijiko kidogo
kimoja hadi viwili vya mafuta haya kila siku kwa majuma kadhaa.
74. Huongeza afya ya figo
Kuanzia kwenye ugonjwa wa figo hadi kwenye mawe ya kwenye figo, mafuta
ya habbat soda yamethibitika kuwa msaada mbadala kwa matatizo ya figo.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa
75. Huimarisha afya ya mbegu za kiume
Ukiacha uwezo wake katika kuongeza stamina na nguvu kwa wanaume na
kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake, mafuta haya pia hutumika
kutibu tatizo la afya dhaifu la mbegu za kiume na kuongeza wingi wake
kwa ujumla (semen count). Kwa mjibu wa tafiti mbalimbali, mbegu za kiume
zinaonekana kuimarika na kuwa nyingi za kutosha baada ya kutumia dawa
hii kwa miezi miwili kila siku.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku hasa habbat soda grade 1
76. Huimarisha mifupa
Tafiti zimeonyesha kuwa mafuta ya habbat soda yanaongeza ukuwaji wa seli
za uboho wa kwenye mifupa kwa asilimia 150 yanapotumika. Hii ni kwa
mjibu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa kwa watu wengi mbalimbali. Kile
kinashangaza zaidi ni kuwa mafuta haya yameonekana kuwa na uwezo wa
kuzuia uongezekaji wa vivimbe mbalimbali walau kwa zaidi ya asilimia 50.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa mwezi mmoja hata miwili.
77. Yanatibu VVU
Matumizi mengine ya dawa hii ya asili yammekuwa ni katika kutibu VVU na
UKIMWI kwa ujumla. Na hapa najua kutakuwa na maswali mengi sana!
Kwa mjibu wa tafiti za hivi karibuni, mafuta ya habbat soda yameonekana
kuwa msaada mkubwa kwa kutibu VVU. Dawa hii ya asili imeleta nafuu kwa
watu wengi kutoka katika dalili mbaya zaidi za ugonjwa huu. Kwa baadhi
ya watu inachukua wastani wa miezi 6 hivi ya matumizi ya habbat soda
kutibu VVU na kutoweka kabisa katika damu na kutokomea mbali kabisa.
Sasa, mimi nimekupa habari na dondoo kwa ufupi, ni juu yako sasa kupeleleza kwa undani jambo hili.
78. Tiba asili ya chango kwa watoto
Ukiwa na mtoto anayesumbuliwa na chango au msokoto wa tumbo linaweza
kuwa ni jambo linalokupa msongo wa mawazo maishani. Ingawa visababishi
vya chango kwa watoto bado havijulikani bayana, kile ambacho
kimethibitishwa ni kuwa mafuta ya habbat soda ni tiba asili kwa chango
au msokoto wa tumbo kwa watoto.
Ni mhimu kuanza na kiasi kidogo sana kama matone matatu hadi matano na uendelee kuongeza kiasi cha dawa kidogo kidogo kila siku.
79. Hurekebisha matatizo katika tezi dume
Afya ya tezi dume ni ishu kwa wanaume wengi duniani kote na kupata dawa
ya asili nzuri kwa ajili hiyo inaweza kuwa mtihani kwa wengi. Kwa bahati
nzuri mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika kwa ajili ya kuimarisha
afya ya tezi dume kwa karne nyingi sasa. Tafiti zinaonyesha kuwa ni
dawa nzuri hata kwa saratani ya tezi dume.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
kwa wiki 4 hadi 6 hasa habbat soda grade 1 (kama yanapatikana lasivyo
hata grade 2 yanafaa).
80. Huondoa udhaifu wa mwili kwa ujumla (lethargy)
Wengi wetu tunapatwa na kupungukiwa na nguvu za mwili wakati fulani
nguvu zote za mwili kwa ujumla na nguvu za ubongo na za kiroho pia. Kwa
ajili ya matatizo ya udhaifu wa mwili iwe kimwili, kiakili na hata
kiroho hakuna dawa nyingine ya asili iwezayo kurekebisha hali hizo kama
yawezavyo kufanya hivyo mafuta asili ya habbat soda.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
81. Huondoa uchovu sugu
Kutoka kwenye maelezo yaliyotangulia hapo juu, mafuta haya pia
yamethibitika kuondoa uchovu sugu wa aina zote na kuupa nguvu mpya
mwili. Matumizi yake ni kama kwenye namba 81 hapo juu.
82. Huhamasisha uzalishwaji wa mkojo
Faida nyingine kubwa ya mafuta ya habbat soda ni uwezo wake wa
kuhamasisha uzalishwaji wa mkojo. Matatizo mengi ya kibofu cha mkojo na
tezi dume yamekuwa yakitibiwa kwa kutumia mafuta ya habbat soda kwa
zaidi ya miaka 2000 sasa na tafiti zimethibitisha hivi karibuni faida
hizi za mafuta ya habbat soda katika majaribio ya kimaabara yakionyesha
kuimarika sana kwa afya ya tezi dume na kazi zake kwa ujumla.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa hasa habbat soda grade 1
83. Huzuia madhara yatokanayo na shambulio la moyo
Kama tulivyoona pale mwanzo kabisa kuwa mafuta ya habbat soda yamekuwa
yakitumika miaka mingi kutibu matatizo mbalimbali ya moyo, vivyo hivyo
yameonekana kuzuia madhara ya pili yatokanayo na shambulio la moyo
(heart attack) na magonjwa mengine kwenye mfumo wa upumuwaji kwa ujumla.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa hasa habbat soda grade 1
84. Husaidia kuongeza damu mwilini
Wengi wetu tunakumbwa na tatizo la kupungukiwa damu (anemia) na hili
linaweza kuiweka miili yetu katika hali ya hatari zaidi. Kwa mara
nyingine tena mafuta ya habbat soda yanaonekana kuokoa tatizo hili baya
la kiafya.
Yamethibitika kutibu tatizo la upungufu wa damu moja kwa moja.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa
85. Huondoa vimelea vya magonjwa
Mafuta ya habbat soda ni kinga dhidi ya vimelea (parasites) vingi vya
magonjwa na huvitafuta na kuviua vimelea hivi popote vitakapokuwa ndani
ya mwili. Hufanya kazi hii kwa kuvilevya hivyo vimelea na kuupa urahisi
mwili kuviangamiza.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa
86. Husaidia kupunguza uzito
Kwa sababu uzito na unene kupita kiasi huhusiana pia na matatizo mengine
ya kutofanya kazi kwa kinga ya mwili, ukaidi wa insulin, kansa na
matatizo mengi katika mfumo wa upumuwaji, ndipo mafuta ya habbat soda
yanapokuja kuwa mhimu kwa ajili ya kupunguza uzito na unene kupita
kiasi.
Mafuta ya habbat soda yamethibitika na watafiti wengi kote duniani kuwa msaada mkubwa kwa wale wanaotaka kupunguza uzito.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
kwa wiki 4 hadi 6 hasa habbat soda grade 1, usisahau pia kufanya mazoezi
ya kukimbia (jogging) kila siku, epuka kukaa kwenye kiti masaa mengi na
ubadili chakula unachokula kila mara hasa uepuke vyakula vya wanga na
vile vyenye mafuta mengi na unywe maji ya kutosha kila siku.
87. Huziua seli za kansa za aina nyingi
Hutibu na kuziua seli za karibu kansa za aina zote, kansa ya mdomoni,
kansa ya ini, kansa ya kongosho nk. Tafiti zimeonyesha mafuta ya habbat
soda kuwa dawa nzuri dhidi ya kansa mbalimbali mwilini kwa kuzuia
uongezekaji wa seli za kansa na kusambaratisha na kansa zenyewe katika
baadhi ya kesi.
Hufanya kazi hii kwanza kwa kuiimarisha kinga yako ya mwili na kuziua seli zenyewe za kansa moja kwa moja.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa mwezi mmoja hadi miwili.
88. Huongeza afya ya ini
Mafuta ya habbat soda yanaimairisha afya ya ini kwa ujumla na kuimarisha
kinga ya mwili. Ni dawa nzuri kutibu matatizo mengi ya ini hata kama
familia yenu wote mna historia ya kuugua ugonjwa wa ini.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa hasa habbat soda grade 1
89. Huondoa sumu mwilini
Tatizo la mwili kuwa na sumu ni tatizo kubwa kwa watu wengi miaka ya
karibuni na kupata mtishamba au dawa ya asili kwa ajili ya kuondoa sumu
bado ni mtihani kwa watu wengi. Kwa bahati nzuri kwa upande wako umepata
mafuta ya habbat soda. Mafuta ya habbat soda yamethibitika kuondoa sumu
kila sehemu ya mwili yanapotumika.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa wiki 4 hadi 6
90. Huondoa hali ya kuchanganyikiwa (Schizophrenia)
Kutokana na sifa yake ya kuondoa vivimbe na sumu mwilini mafuta ya
habbat soda yanaweza kutumika pia kutibu ishara na dalili za
kuchanganyikiwa. Tafiti zimeonyesha mafuta ya habbat soda yakitumiwa na
watu wenye kuchanganyikiwa wanapata nafuu haraka ya tatizo hilo
ukilinganishwa na wale wasiotumia mafuta haya. Matumizi: Kunywa kijiko
kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa hasa
habbat soda grade 1
Hitimisho:
Ni rahisi kuelewa kuwa faida nyingi ambazo mafuta ya habbat soda inazo
zinawashangaza bado watu wengi. Unaweza kudhani hayo hayawezekani kwa
mtishamba wa asili kutoa tiba kwa magonjwa mengi namna hiyo! Kile
ninachojuwa ni kuwa ukweli hujieleza wenyewe.
Kiasi cha faida kinachopatikana katika mafuta haya ukilinganisha na bei
yake ndicho kinachowafanya watu wengi wabaki na mshangao usioisha!
Watu wengi wanashangaa ni kwanini makampuni mengi ya madawa yatumie
mabilioni ya pesa kutengeneza dawa mbalimbali kwa magonjwa mengi ambayo
yangeweza kutibika kwa kutumia mafuta ya habbat soda tu kama tulivyoona
hapo juu.
Ukiacha hayo, kupata hospitali na ukapata matibabu sahihi na kwa gharama
nafuu bado ni changamoto katika nchi nyingi maskini na nyingi ya dawa
zinakulazimu kuendelea kuzitumia kwa kipindi kirefu na pengine bila hata
uhakika wa wewe kuja kupona.
Bahati nzuri kwa wewe ambaye umebahatika kupata habari hizi za habbat
soda na umeweza kuona ni magonjwa mangapi unaweza kutumia kujikinga na
kujitibu nayo.
Na jambo zuri kuliko yote ni kuwa huhitaji kutoka hata jikoni kwako ili
kupata nafuu ya ugonjwa wowote ukiwa na mafuta ya habbat soda karibu
yako.
Mtishamba huu wa ajabu utaendelea kubaki kwenye vitabu vizazi na vizazi
vingi vijavyo kama moja ya tiba asili mhimu zaidi iliyowahi kujulikana
na binadamu.
0 comments:
Post a Comment