Maoni ya baadhi ya wadau wa muziki kuwa kila wanapousikiliza ‘Salome’ wa
Diamond na RayVanny wanapata picha ya matusi, yamekutana na majibu ya
Boss huyo wa WCB.
Akifunguka jana kwenye kipindi cha Ngazi Kwa Ngazi kinachorushwa na
EATV, Diamond alisema kuwa ‘Salome’ haina matusi bali imebeba lugha ya
mahaba mazito.
“Unapozungumzia wimbo wa kimahaba, matusi yanatokea pale. Matusi yapo
kwenye mahaba. Unapokuwa unaelezea masuala ya kimahaba utaonekana kama
unatukana. Lakini sisi tumejitahidi kadri ya uwezo wetu mahaba yale
kuyazungumza katika lugha ambayo ni ngumu sana mtu kuielewa,”
alifafanua.
Kwa upande wake Ray Van, alisema kuwa pamoja na yote yanayosikika kwenye
wimbo ule, wamejitahidi kutumia tafsida kuyaficha na ndio sababu wimbo
ule unapendwa na watu wa rika zote na unaweza kusikilizwa hata katika
jumuiya ya watu wanaoheshimiana.
Salome ni wimbo uliochukua mahadhi ya wimbo wa zamani wa Saida Kalori
‘Chambua Kama Karanga’ na umepata nafasi na mafanikio makubwa katika
vituo vya runinga vya kimataifa na kuweka rekodi ya aina yake kwenye
mtando wa YouTube.
Video ya Salome imeangaliwa zaidi ya mara milioni 13 na laki 7 kwenye YouTube.
0 comments:
Post a Comment