Pages

Subscribe:

Wednesday, March 22, 2017

MAISHA YA CALISAH YAMEKUWA RAHISI BAADA YA KUTOKA KIMAPENZI NA WEMA SEPETU


Mmoja kati ya wachache ambao wanatakiwa kupewa pongezi kwa kukumbuka fadhila ni huyu hapa Model Calisah, kutokana na kuwa muwazi na kufunguka kile ambacho alistahili kukiongea kumuhusu Wema Sepetu.

Ni ukweli usiofichika kwamba ni wachache sana ambao walikuwa wakimfahamu Calisah kabla ya kutoka kimapenzi na mrembo mwenye ushawishi mkubwa sana Barani Afrika Wema Sepetu, kitu ambacho kilimuongezea...
umaarufu mkubwa sana mkali huyo.

Na kufanya Calisah kuwa mmoja kati ya watu ambao walimake headlines kinoma noma kwa Bongo na East Africa kwa ujumla kutokana na mbanga zao ambazo zilikuwa zikiendelea katika mahusiano yao.

Calisah ameamua kuwa mkweli na kufunguka kuwa kutoka kimapenzi na Wema Sepetu kumefungua milango mingi sana ya mafanikio kwa upande wake na kufanya mambo ambayo hata hapo awali yalikuwa magumu kuwa mepesi.

Akiongea Calisah amesema kwamba Wema Sepetu kuna nyota flani hivi amemuongezea ambayo hapo awali alikuwa hana nyota hiyo.

“Nisiwe muongo, kuwa na Wema imeniongezea vitu vingi vizuri, kuna nyota flani ambayo nilikuwa sina nimemegewa yani. Maisha yangu kidogo yamekuwa mepesi kwasababu ya kuwa naye kwasababu kila mtu ambaye alikuwa anamjua yeye Wema, mimi pia alikuwa ananijua. Kwahiyo hii kitu imenisaidia sana. Nina imani hata hii project ambayo nimefanya isinge kuwa Wema isingepata muamko kiasi hiki. Kwahiyo kuwa na Wema imenipa heshima, nimepata mlolongo mwingi sana wa kazi. japo kuwa kuna mabaya mengi lakini sitaki kuyazungumzia naomba tu niishie kwa kusema kuwa kuna mengi mazuri.” Alisema Calisah.

0 comments:

Post a Comment