Pages

Subscribe:

Thursday, March 9, 2017

PLATFOM YA DIAMOND KWAAJILI YA KUUZA NYIMBO ONLINE YAKAMILIKA


Miezi kadhaa nyuma mkali wa Bongo Fleva Diamond Platnumz alitusanua kwamba muda sio mrefu atakuja na mtandao wa kuuza kazi za wasanii. Na kudai kwamba hiyo ni kutokana na wasanii kudhulumiwa sana haki zao na vitu kama hizo.

Hayawi hayawi sasa yamekuwa, mtandao huo umekamilika na tayari kabisa kwa ufanyaji kazi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond Platnumz ametusanua kila kitu kuanzia...
malengo na jinsi ya ufanyaji kazi wa mtandao huo.

Kikubwa na kilichowashangaza zaidi wengi ni baada ya kufunguka kuwa mtandao huo utadeal na kazi za wasanii wengi tofauti tofauti wa hapa nchini, tofauti na matarajio ya wengi kwamba mtandao huo unge-deal na kazi za wasanii wa WCB pekee.

Kupitia post hiyo, Diamond aliandika hivi “Habari Mashabiki zetu pendwa…tunayo furaha kukupa habari njema ya kwamba kuanzia sasa @wasafidotcom ndio sehemu rasmi na pekee ya kuweza kujipatia Nyimbo za wasani wako wote pendwa toka hapa nchini Tanzania na nje ya tanzania…lengo kuu la kuanzisha mtandao huu ni kuweza kuwarahisishia Mashabiki na wadau wa mziki wetu muweze kujipatia kazi za wasani wenu zikiwa zina Quality ama ubora sahihi, kirahisi na haraka…lakini pia kutusapot vijana ama watoto wenu nasi tuweze kuendelea kuwatengenezea kazi zenye ubora zaidi….Lakini pia sababu nyingine ya kuamua kuanzisha mtandao huu ni jinsi mlivyokuwa mnatusapoti vijana wenu kwa kununua kazi zetu halaf mwisho wa siku baadhi ya wamiliki wa mitandao wakawa hawatupi haki zetu tunayostahili, yaani wakawa wanatudhurumu na kunufaika wao huku sie wasanii wenu tukiishia kuambulia umaarufu wa majina ila maisha yetu halisi “pangu pakavu”…hii ilituumiza na kutuliza sana, karibu miaka yote…..kwenye mtandao huu wa @Wasafidotcom tumeeka njia mbalimbali rahisi za kununua nyimbo, kupitia account ya simu yani Mfano: Vodapesa na mitandao yote ya simu Afrika, na pia kununua kwa njia ya Card ya Benki mfano: Master Card, Credit card, Visa card na njia zote za kibenki…. Matumaini yetu kuwa mtatusapoti kwa kununua kazi zetu @wasafidotcom…. na panapo majaaliwa kwa mara ya kwanza ijumaa ya kesho @Harmonize ataachia wimbo wake mpya Uitwao #NAMBIE na utakuwa unapatika @Wasafidotcom tu …. nitasikitika sana sana nikiona ama kusikia shabiki yetu wa damu ama mpemda muziki, anakuwa mtu wa kwanza kuomba kutumiwa nyimbo kwa bloototh ama Watsup badala ya kuingia @wasadidotcom kudownload….. kesho hiyohiyo pia kutakuwa Rasmi na App pamoja na nyimbo za wasanii wengine zaidi uwapendao…. @Wasafidotcom #WhereTheHitsBelong !!!!!! Mie nimewaekea ngoma zooote za tangu kale na zingine ambazo hamjawai kuskia, follow account Rasmi ya @Wasafidotcom ubonyeze link kwa bio ukapakue nyimbo uzitakazo”

0 comments:

Post a Comment