Pages

Subscribe:

Tuesday, October 3, 2017

DAYNA NYANGE: NASUMBULIWA SANA DM NA MASHABIKI ZANGU



Dayna Nyange amefunguka usumbufu anaoupata katika mtandao wa Instagram kutoka kwa mashabiki wake pindi anapochelewa kutoa ngoma mpya. “Huwa wananisema sana mpaka wananifuata DM wanataka na namba za simu, dada mbona huachii nyimbo unafeli” Dayna ameiambia Bongo5.

Muimbaji huyo amesema muda mwingine huwa anapigiwa simu na kufikiri ni show lakini anapopokea anakuta ni mashabiki wake wanaulizia...
wimbo mpya.

Hata hivyo amesema lengo lake la kuchelewa kutoa ngoma ni kwamba anapenda kufanya kitu kizuri ambacho pia kinahitaji maandalizi kwani muziki ni biashara nzuri hivyo ni lazima utumie akili.

0 comments:

Post a Comment