Pages

Subscribe:

Tuesday, October 3, 2017

MADEE: ROMA NI MUONGO ILA NGOMA YAKE NI KALI



Msanii muziki Bongo, Madee amesema wimbo wa Roma ‘Zimbabwe’ ni mzuri ila haamini kama kweli alienda nchini Zimbabwe kama alivyodai wakati ngoma hiyo inatoka. 

Madee ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Sawa’ ameiambai The Playlist ya Times Fm kuwa walijaribu kumuhoji Roma mambo kadhaa lakini hakuwa na majibu yenye ushawishi kitu ambacho...
kinamfanya kutoamini juu safari hiyo.

“Tukajaribu kumuhoji juu uwanja wa ndege wa Zimbabwe unaitwaje akaingia tena chocho, hajatutajia hadi leo, kwa hiyo muongo muongo lakini ngoma yake ni kali kinoma ila yeye sijamuamini” amesema.

“Ila la Zimbabwe siliamini, hilo la kutekwa muache inaweza kuwa kweli ama si kweli, kuna moja ananichanganya yeye kaumia mkono halafu eti anachechemea” ameongeza.

Hata hivyo amesema kuwa muda mwingi yeye na Roma huwa wanapiga stori za kifamilia na utani mwingi na watu wapoona kitu chochote kwenye mitandao kati yao wasikulie serious.

0 comments:

Post a Comment