Pages

Subscribe:

Saturday, March 11, 2017

MSAMI AWEKA WAZI WANAWAKE WA BONGO ANAO WATAMANI



Msanii wa muziki na mwalimu wa dance, Msami Giovani anayefanya vizuri na wimbo wake wa “So Fine”, akiwa amemshirikisha rapper wakike anaye fanya vizuri, Chemical. Msami Baby ameweka wazi hisia za moyo wake na kusema kuna mastaa wa ‘bongo movie’ anatamani kutoka nao kimapenzi.

Msanii huyo amesema katika tasnia ya filamu ametokea kuwapenda wadada watatu ambao ni Wema Sepetu, Elizabeth Michael (Lulu) na Jokate Mwegelo japokuwa amekuwa matatani kwa...
kushindwa kuchagua mmoja kwa kuwa wote ni wazuri.

“Katika Mastaa wa Bongo ambao ninawapenda sana na natamani ningewapata ni pamoja na jokate mwegelo, Elizabeth ‘Lulu’ Michael Pamoja na Wema Sepetu, Nawapenda sana hao wadada na ni wazuri Sana” Alisema Msami kwenye kipindi cha Pillow Talk cha Timesfm.
 
Kwa upande mwingine msanii huyo amesema yeye umri kwake siyo kigezo kikubwa kwakuwa ameshawahi kutoka na mwanamke aliyemzidi umri na wakaishi vizuri bila ya kuwa migogoro ya aina yeyote ile.

0 comments:

Post a Comment