Akiongea hii leo mkurugenzi wa TFDA Hiti Silo amesema kuwa awali
walikamata shehena ya chupa 5,350 za pafyumu zenye thamani ya shilingi
milioni 107 na walipomuuliza mmiliki wa duka hilo Dr Mohamed Gwao
akasema bidhaa hizo zimeagizwa toka nchini Uturuki lakini
walipofuatilia wakagundua zinazalishwa hapa nchini maeneo ya Mbagala
Tuangoma.
Aidha mamlaka hiyo ilipotembelea eneo hilo ilibaini mitambo mikubwa ya kuzalisha pafyumu hizo na kuchukua vifaa vyote kwa ajili ya kuvifanyia uchunguzi zaidi na watuhumiwa wamefikishwa kituo cha polisi.
Mamlaka ya chakula na dawa nchini inawatahadharisha watumiaji wote wa pafyumu hizo kuacha kutumia mara moja kwani bidhaa hizo hazijasajiliwa na TFDA na hivyo ubora na usalama wake haufahamiki.

0 comments:
Post a Comment