Alikiba ameelezea sababu za kwanini rapper wa Nigeria, M.I hakutokea kwenye video yake ya Aje Remix.
Alikiba amesema mara ya kwanza alilazimikia kubadilisha na kuimba
kifaransa sehemu ambayo alikuwa ameimba M.I baada ya ratiba yake kuwa
ndefu, lakini hadi kwenye remix hakufanikiwa hivyo akaamua...
kushoot tu
mwenyewe.
“Hatukutaka kuingilia ratiba zake kwahiyo
sisi tuliweza kufanya ile ya Kifaransa tukamaliza video. Lakini hii ya
sasa hivi vile vile tulijitahidi kwa nguvu zetu zote kuhakikisha M.I
atakuwepo lakini kuna sababu ambazo sisi wenyewe, management yangu ziko
nje ya uwezo wetu,” alisema Kiba.
“Sababu tuliweza kukata tiketi mara mbili,
namaanisha siku mbili tofauti, licha ya kutumiwa tiketi kwa mara ya
kwanza bahati mbaya akakosa ndege na siku ya pili tena ikakosekana
ndege. Kwahiyo kibinadamu tu haipendezi, sio kwamba kuonesha tuna hela
ama nini kwamba tumtumie tena tiketi ya tatu, tukaona haina shida, we
can do this,” aliongeza.
0 comments:
Post a Comment