Pages

Subscribe:

Monday, March 27, 2017

HAYA NDIYO MAONI YA MASTAA WA BONGO BAADA YA TAARIFA ZA KUKAMATWA KWA NAY


Jana march 26 wapenzi wa burudani nchini Tanzania wameamka na habari ambayo siyo nzuri ikihusu kukamatwa kwa msanii wa kizazi kipya Nay wa Mitego.

Huku tetesi zikidai kuwa kukamatwa kwa msanii huyo huenda inatokana na wimbo ambao ulivuja siku chache zilizopita uliofahamika kwa jina la Wapo. Wimbo ambao alisikika rapper huyo Nay wa Mitego na kusemekana kuwa...
ndani ya wimbo huo amewachana viongozi wa serikali.

Jambo hilo la kukamatwa kwa Nay wa Mitego limewagusa wengi hususan wasanii wenzake wa muziki.
Nimekusogezea posts za wasanii 5 ambao wameguswa na tukio hilo na kuamua kuandika katika kurasa zao za mitandao ya kijamii kuhusiana na issue hiyo.

Nikkwapili: Sijui kwanin kakamatwa.....ila kama ni swala la wimbo bora shauri lifanyiwe kazi na basata na sio police.......kama ilivyokuwa kwa nyimbo zingine........namaanisha kama atakuwa amekamatwa kwa sababu ya wimbo.......ila mim sio mjuzi wa sheria labda @albertomsando atusaidie....#free nay 

professorjaytz  :  Naamini sauti ya Mwanamuziki na nguvu ya SANAA inasikika mbali zaidi kuliko hata sauti ya Wanasiasa na ndio maana Wanasiasa wengi wanatumia WASANII kwenye kampeni mbalimbali za kijamii, Tuendelee kupaza sauti zetu bila Hofu, UKWELI UTATUWEKA HURU KWELI KWELI

kalajeremiah  :  nA HAKI ITENDEKE KWA HAKI. SANAA NI KAZI. SANAA INA HAKI YA KUELIMISHA, KUBURUDISHA KUKOSOA NA KUONYA. 

iceboyofficial : #FREENAY BOngo bana Msanii anakamatwa na police kisa Nyimbo. #BINADAMUBwana😀

barakahtheprince:  Mtegemezi wa wanyonge kawa wakuwanyonga wanyonge,kama ni kweli hii kitu...mungu atasimamia.daaah Nchi yangu#TANZANIA #FREENAY

0 comments:

Post a Comment