Ni Mtanzania Jayantilal Keshavji Chande, maarufu zaidi kwa jina la Sir
Andy Chande, ameeleza namna alivyokua kutoka kwenye familia ya kawaida
hadi kuwa kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.
Dar es Salaam. Wamekuwa wakitajwa kwenye kila aina ya minong'ono.
Tumeona matangazo yakialika watu kujiunga nao kama wanataka kupata
utajiri na kuwa watu wenye nguvu. Lakini bado Freemason, imebaki kuwa...
kitendawili miongoni mwa Watanzania wengi.
Leo tunakuletea habari kuhusu Mtanzania maarufu aliyefungua kinywa na
kueleza namna alivyojiunga na Freemasons, kundi lililo kongwe duniani.
Tayari watu mbalimbali watu wenye hamu ya kupata utajiri wamekuwa
wakitoa ushuhuda kuhusu kundi hilo na kusikika kwenye vyombo vya habari,
hasa baada ya kifo cha mwingizaji nyota, Stephen Kanumba, mwaka 2012.
Siyo hivyo tu, bali kumeibuka pia matangazo yenye namba za simu
yanayoshuhudiwa kwenye nguzo za simu mitaani hadi vichochoroni
yakiwataka watu wanaotaka kujiunga na Freemason kupiga simu ili wapewe
utaratibu wa namna ya kujiunga kwenye ‘kisima hicho cha
mafanikio'.
Baadhi ya watu tayari wameshanaswa na mtego huo, huku wengine
wakiendelea kujaribu bahati yao kujipatia utajiri kwa njia ya
‘nguvu za giza'.
Hata hivyo Jayantilal Keshavji Chande, maarufu zaidi nchini kwa jina Sir
Andy Chande, aliyejiunga na Freemason Oktoba 25, 1954 baada ya kupita
kwenye usaili mzito, anaeleza namna alivyoibuka kutoka familia ya
kawaida hadi kuwa kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.
Sir Andy Chande, ambaye amekuwa mwanachama wa kundi hili kwa karibu
miongo sita sasa, anaeleza namna alivyosajiliwa na kufikia hatua ya juu
ndani ya kundi hilo.
Chande alizaliwa Mombasa Kenya, Mei 7, 1928, ingawa wazazi wake walikuwa
wakiishi Bukene mjini, mkoani Tabora, magharibi mwa Tanzania.
Katika kufafanua utaratibu mzima wa Freemason, Chande ameandika kitabu
alichokiita; ‘A night in Africa-a journey from Bukene' (Usiku
wa Afrika-Safari kutoka Bukene), pengine akitaka kuweka sawa dhana na
kuondoa tofauti ili misingi inayoendesha Freemason ifahamike.
Imani ya kimaadili na thamani ya kundi hilo ilianza wakati wa mazungumzo
yake na Messrs Campbell Ritchie na McLean mwanzoni mwa miaka ya 1950.
"Katika kipindi kile nilianza kutambua kuwa Freemason ipo katika msingi
wake. Ni sayansi ya maisha ambayo malengo yake ni kumbadilisha mtu
kiimani na kumfanya awe anavyopaswa kuwa. Ni mabadiliko ya mtu binafsi,"
Sir Andy Chande ameandika katika kitabu chake chenye kurasa 207.
Anasema kuwa malengo ya Freemason yamefunikwa na mafumbo, ambayo pengine
ndiyo yanayoeleza utamaduni uliojificha katika utendaji kazi wake.
Chande anabainisha kuwa kanuni kubwa tatu za Freemason ziliandikwa
kwenye kitabu kimoja nchini Canada, kilichochapishwa na Kampuni ya
Penumbra Press.
Anaandika: "Kwa hiyo, ukiwa kwenye ngazi ya kwanza (first degree),
kanuni inayoongoza, inamtaka mtu awe mkweli na mwenye maadili ambayo
hasa Freemason inalenga kuyaweka kwenye akili, ili mwanachama awe mzuri.
Ngazi ya pili ya utaratibu inatilia mkazo kwenye vipaji na akili kupitia
sanaa na sayansi, ili kutoa mchango mzuri iwezekanavyo kwenye maisha."
Anafafanua kuwa ngazi ya tatu inampa mtu nafasi ya kutafakari uwepo wake
kwa kina na kwamba kanuni zote tatu zinafahamika kama upendo wa
kindugu, kujiweka huru na ukweli.
"Kwa njia hizi inamaanisha, unafundishwa namna ya kuyafurahia maisha kwa
kiwango chake cha juu. Kwa kufuata hizo kanuni tatu za upendo wa
kindugu, kujiweka huru na ukweli, wakati huohuo ukijitambua na kuanza
kujiandaa na kutokwepeka kwa kifo," anaandika Chande.
Anaongeza kuwa, wakati kanuni hizo tatu zinapoondolewa kwenye alama ya
sanaa inayofunika imani ya Freemason, ambazo zilimpa udadisi wa kupata
taarifa kuhusu utaratibu huo wa kale.
Sir Andy Chande ni Kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.
Kanuni za Freemason zinafundisha nini?
Katika ratiba ya Freemason, anaandika Chande akieleza kuwa, kanuni ya
upendo wa kindugu inawafundisha ndugu wote kuwachukulia wanadamu wote
kama familia moja iliyoumbwa na nafsi moja kuu.
"Kujiweka huru, vilevile, inaleta ujumbe nilioupata kutoka kwa baba
yangu, aliyesema ni kuwekwa huru kwa mtu mwenye msongo. Kama ni kuwekwa
huru kutoka kwenye umaskini, matatizo au akili isiyo na furaha,"
anaandika Chande katika kitabu hicho.
Anafafanua kuwa ngazi ya tatu ambayo ni ukweli na pengine ndiyo muhimu zaidi ni mchango wa kimungu kwa mwanachama wa Freemason.
Anabainisha kuwa kipindi hicho ndicho kinachoheshimika kama njia ya
matazamio na marekebisho na kama inawezekana, kurudiwa kwa kanuni hizo
kama msingi wa kuelekea kanuni kuu nne alizozitaja kuwa ni; udhibiti
binafsi, nguvu, umakini na haki.Chande anaeleza kuwa Freemason siyo
kifaa cha dini, pia siyo mpinzani wa dini, lakini inakaribisha watu wote
bila kujali dini zao na haijaribu kubadilisha imani zao au kushawishi
kuabudu kwao.
"Inajaribu tu kuwafanya watu kuwa wema," anaandika Sir Chande akifafanua:
"Hii ndiyo dunia niliyoingizwa mwaka 1954, imekuwa na mchango mkubwa
katika maisha yangu tangu wakati huo…: Roho yangu, akili yangu
na nafsi yangu, vimetajirishwa na kushiriki kwangu Freemason
0 comments:
Post a Comment