Monday, March 27, 2017
MR NICE AWEKA WAZI SABABU ZILIZO MFANYA KUKIMBIA BONGO
Huwezi kuwataja wakongwe waliofanya poa kipindi cha nyuma kwenye muziki wa Bongo FLeva ukaacha kumtaja Mr Nice.
Kwasababu ni mmoja kati ya wakongwe ambao walifanikiwa kuwa na fanbase kubwa sana kipindi cha nyuma, ila ukweli usiofichika ni kwamba mkali huyo kwasasa hana tena...
nguvu kama aliyokuwa nayo zamani kwa hapa nchini.
Mwandishi ameona sio kesi kama ikimtafuta Mr Nice na kupiga naye story kuhusu muziki wake na mambo mengine kibao. Na tumefanikiwa kuzungumza mambo mengi sana na mkali huyo ikiwa ni pamoja na maisha yake, muziki wake na vitu kama hivyo.
Mr Nice amwambia mwandishi kwamba kwasasa ameamua kuhamishia makazi yake nchini Kenya, kwasababu ndio sehemu ambayo anaona anapata heshima kama msanii tofauti na Tanzania.
Pia Mr Nice amefunguka kuwa nchini Kenya ndio sehemu ambayo ana mashabiki wengi na muziki wake anaufanya poa kabisa na hata akiwa na show anapiga nyomi kama kawiz.
Mr Nice amenitumia baadhi ya picha za matukio yake kimuziki ambayo anafanya nchini Kenya, ikiwa ni shows, love ya mashabiki zake nchini humo pamoja na mambo mengine kibao.
.
.
. . . . . . . .
“Hizi ni baadhi za maujazo yangu huku bro ..maisha yanaendelea vyema kabisa … Hizi ni show ambazo huu ujazo woote ni wangu bro ,si kwamba ni show ambayo iko na wasanii wengine hapana ..ndiyo maana kiburi inakuwa mob kwa kichwa …ila tuko pamoja sana,nikikuja bongo nitakutafuta ,huwa nakujaga mara moja kusalimia wazazi na kugeuza” ALiniandikia Mr Nice.
Pia tuliongelea mafanikio ambayo ameyapata kwa biashara yake ya muziki pande hiyo ya 254, Mr Nice hakusita kunipa list ya mandinga ambayo anamiliki pande hizo.
“Niko na bmw sports comvetable na ,x-trail na elgrand nissan new shape ..hizi kubwa ni kwa ajili ya kuendea mashowz huko mbali na sometimes mavijijini si unajua kunakuwa ni rough road so 4w-drive inahusika ..haka ka bmw ni kakupigia race town .
Hizi ndo heshma na maisha ninayopewa huku bro …na hata wasanii wenzangu wa huku wananiheshimu na kunipenda mbaya kabisa” Aliniandikia Mr Nice kupitia Mtandao wa Whatsapp
Pia Mr Nice alifunguka sababu zinazomfanya ashindwe kukaa Bongo na kuamua kulowea nchini Kenya na kujisikia ndio sehemu ambayo yuko salama zaidi.
“Tofauti ya nchi za wenzetu na hapo bongo ,bongo unafki majungu na fitna ndiyo zinarudisha kila kitu nyuma kaka ..huku kwa wenzetu mambo hizo hakuna kabsaaaaa …so am more safe and comfortable here coz hata viongozi wa serikali wananipenda sana na kunipa sapoti kuliko hata hapo home tz .mi now nikija tz nakuja kusalimia familia yangu na fans wangu sugu tu huko lakini sitarajii kufanya kaz yoyote ile tena bongo nimevunjwa moyo sana hasa na serikali kutokujali mchango wetu wasanii .hata show bongo sitaki ndo maana hata album yangu mpya ya kioo sikushuhulika kuileta huko maana sikuona kama inaweza saidia lolote.” Alisema Mr Nice.
Bonyeza play kwenye video hii hapa chini kusikiliza exclusive interview ambayo nimefanya na Mr Nice kupitia njia ya simu na kuzungumza mambo mengi kinoma noma.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment