Wanawake
wana siri nyingi sana mioyoni mwao na kwa kawaida huwa hawawezi
kuonesha hisia zao za ndani moja kwa moja. Ni watu ambao mara nyingi
hupenda kuwasilisha vilivyomo ndani yao kwa ishara.
Kwa
mtindo wa maisha ya wanaume wengi wa sasa ni vigumu kusoma ishara hizo
na kujua mahitaji ya mwanamke husika. Bahati mbaya ni kwamba, ukienda
kinyume na mahitaji yao, utashangaa kila siku mnaingia kwenye...
mikwaruzano isiyo na msingi.
Wiki
iliyopita nilieleza machache, leo tunaingia katika sehemu ya mwisho.
Hebu fuatilia kwa makini ujue mwanamke anapenda vitu gani hasa ili uweze
kuishi naye kwa amani.
KUSIKILIZWA
Ukitaka kumpatia mwanamke, msikilize. Kumbuka wanawake wengi wana hulka ya kuongea sana! Ndivyo walivyo.
Wakati fulani, mwanamke anapenda kuzungumza mambo fulani na mwanaume wake.
Pengine
anapenda kumshauri au kujadiliana naye jambo fulani; huenda ana mawazo
mazuri lakini mtindo wao wa kuongea sana unaweza kukatisha tamaa.
Usifanye hivyo. Mpe nafasi.
Msikilize
kwa makini, mwishowe unaweza kupata manufaa makubwa kutokana na maneno
yake. Amini usiamini, hata katika mambo yanayohusu mafanikio,
ukimshirikisha mkeo, huwa na mawazo mazuri yanayochochea kuifukuzia
ndoto yako.
Ukiachana
na hilo, mwanamke anaweza kukuambia, hapendi mavazi yako – hapendi nguo
fulani unayovaa, labda kwa hoja kuwa haikupendezi! Usimdharau. Sikiliza
hisia zake.
Kumbuka
upo kwa ajili yake, anaweza kujiuliza, kama anakuambia mavazi hayo si
mazuri kulingana na umbo lako na ung’ang’ania, unamvalia nani huko nje?
Msomaji mmoja aliwahi kuniambia: “Yaani kaka Shaluwa, mume wangu
ananishangaza sana.
“Anapenda
kuvaa suruali za vitambaa, pana na mashati makubwa kama Mzaire.
Nimeshamwambia mara nyingi kuwa sipendi na hapendezi, lakini bado
analazimisha kuvaa. Ananinyima raha sana, maana hata nikiongozana naye,
nakuwa kama nipo na mtu mzima!”
Unaweza kuona namna gani wanawake wanavyokereka na mambo madogo tu lakini wakiyapa uzito
wa hali ya juu.
MSIMAMO
Wanawake
wanapenda mwanaume mwenye kujiamini na kusimamia msimamo wake. Unaweza
kushangaa lakini wakati mwingine mwanamke anaweza hata kukuweka kwenye
mtego; mnakubaliana jambo lakini baadaye anajifanya kukupinga ili kuona
msimamo wako.
Wanaamini
katika mwanaume anayejielewa na asiyeyumba wala kuyumbishwa. Kwamba,
mwanaume wa aina hiyo ni rahisi kufikia ndoto za familia – yeye kama
kiongozi wa nyumba.
ZAWADI
Si
lazima ununue gari jipya na kumpelekea kama zawadi. Kumchagulia wimbo
mzuri redioni, kadi yenye mashairi mazuri ya kimapenzi, bangili,
vipodozi na vitu vingine vidogovidogo huwafurahisha sana wanawake.
MTOKO
Hata
kama ni mara moja baada ya miezi miwili, ukitoka na mwenzako na kwenda
naye kupata chakula cha jioni mgahawani huongeza mapenzi. Kwa mwanamke
ni jambo kubwa lenye thamani sana.
0 comments:
Post a Comment