Msanii Mrisho Mpoto amewaomba
wanasiasa waachie ‘gap’ kidogo ili wasanii nao waweze kupata muda wa
kutambulisha kazi zao za sanaa kwa jamii ambayo sasa imetekwa na upepo
wa siasa.
Hayo
yameibuka kutokana na matukio makubwa ya kisiasa kila kukicha na baadhi
ya wasanii wakiongozwa na Mpoto kuandika katika mitandao ya kijamii
kuwataka wanasiasa wajaribu kidogo kupunguza...
kasi yao ili nao waweze
kusikika.
“Mtu amewekeza hela nyingi
na anajaribu, anakuta hakuna ‘gap’ kwenye soko kwa sababu macho, mawazo
yote ya watu yamehamia katika siasa. Kwa hiyo nikasema hii ni hatari
kwasababu unaweza sema labda kesho, keshokutwa patatulia, mtondo,
mtondogo patatulia, unaichukulia kama mzaha vile lakini sasa unaona kila
kukicha kuna ‘breaking news’ kwa hiyo nikasema hapana tafadhari kidogo
watupe ‘gap’ kidogo ili watu waweze kufanya ‘promotion’ za nyimbo zao”. Alisema Mrisho
Aidha msanii huyo amesema siyo kweli
kwamba wanasiasa hawaelewi chochote wanachowafanya wasanii na watu
wengine wanaotegemea upepo wa ‘promo’ katika kufanya na kutangaza kazi
zao.
“Wanasiasa wenyewe wanajua
leo tukiamshe kipi siyo kwamba hawajui wana-strategy kabisa kesho
tuamshe hiki keshokutwa tuamshe kile”. Alisisitiza Mpoto
Vile vile Mjomba amesema kwa sababu
wanamsikia anawaomba kidogo ‘slow down’ ili vijana wao waweze ku-boost
kazi zao kwa sababu ‘investment’ kubwa wameweka katika hizo shughuli,
muda pamoja na fedha.
0 comments:
Post a Comment