Pages

Subscribe:

Sunday, March 5, 2017

QS MHONDA: NITAENDELEA KUWASAIDIA WASANII



QS Mhonda amefunguka kuwa ataendelea kuwasaidia wasanii japo amepata hasara ya takribani milioni 200 kutoka kwa Q Chief. Bosi huyo ambaye pia ni mmiliki wa lebo ya QS Mhonda ambayo ilikuwa inamsimamia msanii huyo amesema alijua tangu mwanzo kuwa hili litatokea kwake kwa kuwa tayari watu wengi walimuambia awe makini na Chillah kwa kuwa ni msumbufu sana.
 
“Nisema tu, hili lililotokea siyo kama litanivunja moyo kuwasaidia vijana wengine nitaendelea kusaidia kama kawaida. Nilijua hili tangu mwanzo kuwa litatokea kwa kuwa...
watu wengi waliniambia kuwa Q Chief ni msumbufu na ninajua haya yanatokeaga kwa wasanii,” QS amekiambia kipindi cha FNL cha EATV.

Bosi huyo ameongeza kuwa iwapo siku Q Chief atahisi amemkosea basi amfuate amuombe radhi na kama yeye atahisi siku mmoja amemkosea msanii huyo atamfuata na kufanya hivyo.

0 comments:

Post a Comment