Pages

Subscribe:

Sunday, March 5, 2017

TIMBULO: MWANAMKE AKINIOMBA PESA SIMPI BORA NIITUME KWA MAMA


Mzee wa kugoogle ukipenda muite domo zege Timbulo baada  ya kuacha kazi ya kufundisha  aliamua zake ajikite kwenye industry ya Muziki japo Mama yake hakupenda hata kidogo.

Unaambiwa kipindi Domo zege inatoka Jamaa alikuwa ameshapoteza direction kabisa na kurudi zake home kwao Mbeya akamsaidie mama yake kuchunga ng’ombe na...
shughuli nyingine za kilimo.

Ndipo Mungu akabariki hustle zake leo hii anasumbua jiji kwa ndinga kali na hits yake ya USISAHAU ikitesa kwenye station  za Radio na Television Bongo na Afrika nzima.
Kitu ambacho  hawezi kukisahau maishani siku ambayo Alipigiwa Simu na Suka wa Clouds kuhusu ngoma yake ya Domo zege anahitajika kwenye Interview na anatakiwa aje Bongo.

Anachokumbuka ilikuwa usiku wa manane lakini alipomueleza mama yake kuhusu jambo hilo alimkopea pesa kwa majirani akapata nauli ya kuja  Dar es salaam.
Mjamaa anasema yeye ni mbahili sana Kama demu akimuomba pesa Kama pesa hiyo anayo bora akamtumia mama yake tu, mshikaji anampenda Mama yake kuliko kitu chochote unaambiwa.
Yeaah man Baraka zote ni kwakina mama wote ambao wametufanya tufike hapa.

0 comments:

Post a Comment