Pages

Subscribe:

Thursday, September 6, 2018

KANYE WEST AAMUA KUJISHUSHA NA KUOMBA MSAMAHA KWA DRAKE

Rappa Kanye West ajishusha na kumuomba Drake msamaha kupitia ukurasa wake wa twitter hii ni baada ya diss aliyoitoa Drake kwenye ngoma aliyoshirikishwa na French Montana .

Kupitia msamaha huo aliouomba Kanye amegusia vitu vingi ambavyo vilisababisha kuwepo na tofauti kati yao ikiwemo ishu ya kuingilia mwezi ambao Drake alitakiwa kutoa album yake ya ‘Scorpion’ mwezi June na yeye ndipo...
alipopanga kutoa album zake tano mwezi huo huo.

Kanye West ameongelea pia ishu ya kuachia ngoma ya “Lift Yourself” mwenye bila kumshirikisha Drake ikiwa walikuwa wanampango wakushirikiana pamoja kwenye ngoma hiyo.

Kanye ameongeza na kusema kuwa hawezi kuingilia mambo ya familia hivyo hakumuambia chochote Pusha T kuhusiana na mtoto wa Drake aliyetajwa kwenye ngoma ya Pusha T  “Story Of Adidon” kama ilivyosemwa na amesema kuwa atahudhuria show ya Drake siku 7 zijazo kumpa mapenzi na kukubali ubunifu anaoufanya.

D

0 comments:

Post a Comment