Pages

Subscribe:

Saturday, February 18, 2017

ALIKIBA AFIKISHA MALALAMIKO YA MASHABIKI KWA WADHAMINI WAKE

Alikiba ameyasikia malalamiko ya mashabiki wake kuhusu ukimya wake wa hapa na pale na amekiri huumia sana kuona wakimrushia lawama. Kutokana na ukweli huo, hitmaker huyo wa Aje amedai kuwa amelazimika kuwaambia mabosi wa Sony kuwa wajipange vyema ili kuhakikisha kuwa mashabiki wake wanaridhika.

Kwenye interview na millardayo.com, Alikiba amedai kuwa CEO wa Sony Music Africa, Sean Watson, ameiambia bodi ya label hiyo jinsi Alikiba alivyo na... mashabiki wengi nyuma ambao panapotokea kuchelewa kwa lolote, ‘hung’ata kama nyuki.’

“Kwahivyo they have to make sure kila kitu kinaenda on point, kila kitu hakitakiwi kudelay, kila kitu kinakwenda sawa,” amesema Kiba.

0 comments:

Post a Comment