Pages

Subscribe:

Saturday, February 18, 2017

HII NDIYO SABABU YA RAY C KUZIMIKA KWA RAYVANNY


Msanii mkongwe wa Bongo Fleva Ray C ni moja ya wasanii wanaomkubali sana Rayvanny kutoka WCB na sio tu kwa staili yake ya uimbaji bali pia anavutiwa sana na uandishi wake wa Mashairi.

Ray C amesema Rayvanny bado ni mdogo kiumri lakini kwa alipofikia na uwezo wake wa utungaji wa mashairi bila shaka yoyote atafika mbali sana kwenye muziki kwani hata yeye kwa sasa anatamani... kufanya nae kazi.

“Nampenda sana yule mtoto Rayvanny, anaandika sana mashairi, nasikia anaandikia wasanii wengi nyimbo, hata mimi natamani kufanya naye kazi na naamini atafika mbali sana kimuziki” alisema Ray C kwenye mahojiano yake na Kituo cha East Africa Radio.

Hata hivyo Ray C kwenye mahojiano hayo amewaahidi mashabiki wake kuwa amejipanga vilivyo kurudi kwenye Game kwani anajua nafasi yake kwenye muziki bado ipo.

0 comments:

Post a Comment