Pages

Subscribe:

Wednesday, August 22, 2018

MBWA APELEKEA KIFO CHA MWANADADA KULIWA NA MAMBA



Mwanamke mmoja nchini Marekani ameuawa na mamba mwenye ukubwa wa futi nane maarufu kama ‘alligator’ baada ya kutaka kumsaidia mbwa wake aliyekuwa anapiga kelele pembezoni mwa bwawa.

Victim Cassandra Cline mwenye umri wa miaka 45, ameuawa na mamba huyo kisha kumzamisha hadi chini ya maji wakati alipokuwa....
akifanya jitihada za kumsaidia mbwa wake huko South Carolina Marekani.

Polisi wa jiji hilo wamesema kuwa mamba amemshambulia mwanamke huyo akitokea kwenye bwawa hilo linalopatikana karibu na nyumba.

Inaelezwa kuwa kuna ripoti ya kifo kimoja tu kuwahi kutokea kinacholingana na hicho katika eneo hilo la South Carolina kwa zaidi ya miaka 42.

Alligator ni aina ya mamba wakubwa kabisa duniani ambao wanauwezo wa hali ya juu wanaopatikana kwenye nchi za Marekani na China.

0 comments:

Post a Comment