Pages

Subscribe:

Wednesday, August 22, 2018

UWOYA AZUNGUMZIA UKARIBU WAKE NA TESSY WA ASLAY


Msanii wa filamu Irene Uwoya amefunguka kuzungumzia ukaribu alionao na aliyekuwa mpenzi wa muimbaji Aslay, Tessy.

Muigizaji huyo ambaye ni mke halali wa rapa, Dogo Jana amedai yeye akikutana na mama watoto huyo wa Aslay hawazungumzi ishu kuhusu...
wanaume zao.


“Ni mtu ambaye tukikutana tunazungumza mambo ya biashara, lakini ishu zake za mapenzi huwaga sizijui, pia ishu kuhusu mahusiano yake ni privacy, huwa nikikutana naye hatuzungumzi masuala ya mapenzi kwa kwa sababu kila mtu ana wake,” alisema Uwoya.

Aliongeza, “Sijui kwa sasa yupo na nani kwanza hayanihusu kabisa”
Tessy ambaye alibahatika kuzaa mtoto mmoja na Aslay, anadaiwa kutoka kimapenzi na mfanyabishara mkubwa nchini Tanzania aitwae, Sebastian Ndege.

0 comments:

Post a Comment