Pages

Subscribe:

Monday, May 7, 2018

FAIZA ALLY AMWAGA MACHOZI HADHARANI BAADA YA KUNASA UJAUZITO TENA

Faiza Anasa Mimba Nyingine  Amwaga Chozi Hadharani
Mwigizaji wa sinema za Kibongo ambaye ni mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) anayetumikia kifungo cha miezi mitano jela, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally amejikuta akimwaga machozi laivu!

Kwa mujibu wa chanzo makini, hivi karibuni Faiza alinasa ujauzito mwingine wa mtoto wa tatu huku mtoto wake wa pili akiwa na umri wa miezi nane tu kisha ukachoropoka. Chanzo hicho kilitiririka kuwa, Faiza alianza kuumwa bila kujua anaumwa nini baada ya... kuwa anatumia dawa akiamini ni za kuzuia ujauzito, kumbe zilikuwa ni za kuharibu mimba.

Ilisemekana kwamba, Faiza alifikia hatua ya kutumia dawa hizo akiamini hatapata mimba kwa kuwa baba wa mtoto wake wa pili alikuwa amekuja Bongo kwa kuwa ni raia wa Marekani. Kiliendelea kutiririka kuwa, Faiza alikuwa haelewi, lakini kila alipotumia dawa hizo alipata maumivu makali na kuanza kuona mabadiliko makubwa kwenye mwili wake, hasa wakati wa hedhi.

Ilisemekana kwamba, kufuatia hali hiyo, ilimlazimu Faiza kwenda kuonana na daktari ili kujua ni kitu gani kinamsumbua. “Alipoamua kwenda hospitalini alikuwa hajui tatizo ni nini kwenye mwili wake. Kila alipokuwa akitumia dawa hizo zilimfanya ajisikie vibaya mno.

“Pale kwenye Hospitali ya AAR ndiyo waligundua kuwa alikuwa na ujauzito ila ulishaanza kutoka na kubaki masalia ambayo ilibidi asafishwe,” alitonya mtoa ubuyu wetu. Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa, baada ya kugundulika kwamba alikuwa na ujauzito, lakini ukawa umeharibika kutokana na dawa hizo, madaktari waliamua kumsafisha ili kumrudisha kwenye hali yake ya kawaida.

0 comments:

Post a Comment