Pages

Subscribe:

Monday, May 7, 2018

MADJ NCHINI MAREKANI WAGOMA KUPIGA NYIMBO ZA KANYE WEST


Tokeo la picha la Kanye west
Kauli ya Kanye West aliyoitoa wiki iliyopita kwenye mahojiano yake na mtandao wa TMZ akidai kuwa “Watu weusi walichagua kuishi kama watumwa kwa miaka 400“. Huenda ikawa imepokelewa kwa huzuni na jamii ya watu weusi nchini Marekani kwani tayari MaDj wawili wa kituo maarufu cha radio cha 105.1 The Bounce mjini Detroit wamekataa kucheza ngoma zake kwenye kipindi chao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa rasmi wa Facebook wa kituo hicho cha Radio, MaDj hao maarufu mjini Detroit,  DJs BiGG na Shay Shay Say  wamesema kuwa...
wamefikia maamuzi hayo baada ya kuona kuwa maoni aliyotoa Kanye West kuwa watu weusi walichagua kuwa watuma yamefika mbali sana.

“Imetosha kwa sasa, hatutaki tena kusikia wala kucheza nyimbo za Kanye kwenye kipindi chetu, hatutamzungumzia tena Kanye West. Kwa hili tunasimama wima kwa pamoja na hatutacheza nyimbo zake, tumekataa kumpa platform kabisa.“imeeleza taarifa yao waliyoitoa MaDJ hao.

Rapa Kanye West mnamo Mei 01, 2018 akiwa kwenye mahojiano na mtandao wa TMZ alinukuliwa akisema kuwa “Watu weusi walichagua kuwa watumwa kwa miaka 400” .
Soma zaidi – Chris Brown amchana Kanye West kupitia mahojiano ya Will.i.am
Hata hivyo, Kanye West bado ameendelea kutetea maoni yake kupitia ukurasa wake wa Twitter akidai kuwa alimaanisha kwa kizazi cha sasa cha jamii ya watu weusi kuishi na mawazo hayo ya kutawaliwa miaka ya nyuma ni utumwa pia.

0 comments:

Post a Comment