Pages

Subscribe:

Thursday, May 25, 2017

BEN POL AFUNGUKA SABABU ZA KUPIGA PICHA ZA UTUPU



Baada ya Ben Pol kuchafua hali ya hewa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia Alhamisi ya wiki iliyopita kutokana na picha zake zinazomuonyesha akiwa nusu mtupu kuenea mitandaoni na kumsababishia kukutana na mvua kubwa ya matusi, msanii huyo amefunguka sababu ya kufanya hivyo.

Muimbaji huyo ambaye ameachia wimbo wake mpya ‘Tatu’, ameiambia Bongo5 Junanne hii kuwa alifanya hivyo ili kuendana na...
kasi ya biashara ya muziki ambayo amedai kwa sasa inahitaji matangazo.
 
“Ile picha unajua muziki umebadilika na unataka kufanya promotion ya kitu chako unatakiwa kutoa material zote ya project yako. Sasa mimi nilikuwa anatoa wimbo ambao unazungumzia ufungwa, mtu ambaye hana uhuru, hawezi kusema,” alisema BenPol. “Kwahiyo mimi nimefanya hivyo ili kuwakilisha kile kitu ambacho nimekifanya ndani ya wimbo, sikuona kama nina sababu na kufanya kitu tofauti wakati kuna njia moja ya kupita ili kufanikishha jambo langu,”

Hatahivyo muimbaji huyo amedai hakufanya vile ili kutafuta kiki kama baadhi ya watu wanavyodai kwenye mitandao ya kijamii.

0 comments:

Post a Comment