Pages

Subscribe:

Wednesday, May 31, 2017

WAKAZI: ALBUM YA KISIMANI HAIJACHAHA



Msanii wa muziki wa hip hop, Wakazi, anajipanga kuachia albamu yake mpya ‘Kisimani’ ndani ya mwezi huu wa Ramadhani baada ya kuiandaa kwa kipindi cha miaka mitano.

Rapa huyo amedai tayari ameshawaahidi sana mashabiki wake juu ya albamu hiyo lakini kwa sasa analazimika kuiachia kwa namna yoyote, Akiongea na Bongo5 wiki hii, Wakazi amedai alikuwa anashindwa kuiachia albamu hiyo kutokana na...
ratiba za kazi zake kuingiliana.
 
“Nimewaahidi sana mashabiki kuhusu albamu lakini kwa sasa sitaki tena kutoa ahadi, miaka mitano imetosha. Haijachacha kwa sababu kila siku naongeza vitu vipya, tena ndio imezidi kuwa kali zaidi,” alisema Wakazi.

Aliongeza,”Mungu akipenda mwezi huu wa Ramadhani naachia albamu ya Kisimani kwa sababu kundi letu pia litaachia albamu. Kwahiyo nilitaka nianze kwanza kuachia hiyo albamu then ndio itoke ya kundi,”

0 comments:

Post a Comment