Pages

Subscribe:

Friday, May 26, 2017

HIKI NDICHO WALICHO KIFANYA G NAKO NA BELLE 9 KWAAJIRI YA HARUSI


Wasanii G Nako na Belle 9 katika project yao mpya ‘Ma-Ole’ ni kwa ajili ya kusherehesha kwenye harusi, na ni mwanzo wa kuwaandikia maharusi nyimbo kwa wale watakaohitaji.

Belle 9 amesema wakati wanatoa wimbo ‘Give It To Me’ akiwa na G Nako walipata show kadhaa za pamoja ambazo walienda kufanya kwenye harusi tofauti tofauti ndipo wakawaza kuja na...
wazo jipya la kutengeneza pesa kupitia harusi.

“Ma- Ole maana yake  ni My Only kwa kingereza, kwa sababu hii tumeudedicate moja kwa moja mtaani kwa watu wa kawaida, kwa mashabiki wetu kama watakuwa na harusi. Mimi na G Nako kwa sasa hivi tunaandika stori yako na mtu wako toka mmekutana, mnatuelezea tunaandika halafu tunakuja kuperform kwenye harusi yako ,” amesema Belle 9.

0 comments:

Post a Comment