Pages

Subscribe:

Wednesday, July 26, 2017

NIKKI WA II: TANZANIA KUNA UTAMADUNI WA KUWAPANGIA VIJANA

Msanii kutoka kampuni ya Weusi Niki wa Pili amewapa ushauri vijana waliozaliwa katika ardhi ya Tanzania kwa kuwaambia waache kufuta mifumo au mitazamo isiyo akisi katika ujana wao na badala yake wajitume katika kupambana na hali ya maisha ili waweze kufanikiwa maisha kabla ya miaka 38.

Nikki amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kuwepo kundi kubwa la vijana mtaani huku wengine wakiamini kwamba hawawezi kufanikiwa maishani mwao mpaka wawe na...
mtu pembeni yao wa kumpa msaada wa kumshika mkono ili aweze kufika mahali fulani.

"Tanzania kuna utamaduni mkubwa wa kuwapangia vijana cha kufanya, kusema hata kuvaa. Huko mashuleni au vyuoni sauti za vijana, wanafunzi hazina nafasi katika kuandaa mitaala wala namna ya kuendesha vyuo au shule kila kitu kinapangwa na walio wakubwa zaidi ndiyo maana kufanikiwa wengi wanaanza juu ya miaka 38", ameandika Nikki wa Pili.

Pamoja na hayo, Nikki ameendelea kwa kusema "Vijana msifuate mifumo au mitazamo isiyo akisi ujana wenu, nguvu yenu na ndoto zenu. Msisubiri vitoke juu kwa wakubwa kama msaada, anzieni chini mjifunze kupitia nyie kwa nyie", amesisitiza Nikki.

Kwa upande mwingine, Nikki amesema hata katika madarasa ya elimu ya juu (masters) hakuna uhusishwaji wa sauti za wanafunzi katika kufanya jambo lolote lile ila kinachoangaliwa ni jinsi gani umelipa karo ya masomo na kuingia darasani na kufundishwa tu.

0 comments:

Post a Comment