Pages

Subscribe:

Monday, July 31, 2017

MSAGA SUMU AAMUA KUMCHANA MAKAVU DULLA MAKABILA

Mfalme wa kisingeli Tanzania, Msaga Sumu amefunguka kwa kumtaka Dulla Makabila aache tabia ya kuweka tamaa mbele kwa madai anachokifanya kinaweza kuwaaminisha watu kuwa waimba singeli wote ndivyo walivyo. 

Msaga Sumu amesema hayo baada ya Dulla Makabila kuwa na tabia ya kuchukua 'show' mbili kwenye usiku mmoja katika mikoa tofauti jambo ambalo...
ni kinyume na taratibu za ujuzi wake anaoufanya kwa maana anakuwa anawadanganya baadhi ya eneo.  

"Nimeshaletewa mashtaka mengi kwa mambo anayoyafanya mdogo wangu Dulla, siyo mara ya kwanza, nimeshamuweka chini kuongea naye mara nyingi tu. Huwa namwambia kuwa mkweli katika jambo moja, unapokuwa na tamaa utajiaribia halafu muziki utakuja kuuwa kisha tutakuja kuonekana watu wote tunaoimba singeli ndiyo tabia zetu zipo hivyo kumbe tofauti kabisa", amesema Msaga Sumu.

Pamoja na hayo, Msaga Msumu amesema siri pekee ya kufanikiwa katika muziki ni kuwa na nidhamu jambo ambalo linapelekea kupendwa na watu wa rika zote hata kama utakuwa hujui kuimba.

"Ukiwa na nidhamu na heshima katika muziki unaishi miaka mingi sana na kujuana na watu tofauti. Utapendwa kwa sababu ya nidhamu pia nidhamu yako inaweza kukifikisha mbali. Siku zote huwa namwambia mdogo wangu Dulla awe na nidhamu na ache kauli za kavu kavu maana kuimba na kuongea ni tofauti", amesisitiza Msaga Sumu.

Katika hatua nyingine, Msaga Sumu amesema ataendelea kubakia kuwa mfalme kwa madai katika nchi moja hapawezi kuwa na wafalme wawili hata siku moja huku akiendelea kufafanua kuwa wasanii wa sasa hawana ubunifu ndiyo maana sasa wamefeli katika muziki wa singeli wanaofanya.

0 comments:

Post a Comment