Pages

Subscribe:

Tuesday, July 25, 2017

FID Q AKIRI KUWA RICH MAVOKO NI MOTO WA KUOTEA MBALI


Kama bado hujapata nafasi ya kukitazama kichupa kipya cha Rich Mavoko pamoja na Fid Q cha “Sheri” basi utakuwa umekosa mavitu flani hivi ya kinyama, tena mbaya zaidi kama hujakaa na kuisikiliza hii ngoma vizuri basi hutoelewa Fid Q alichomaanisha kwenye Tweet yake.


Sheri, ni ngoma ambayo iliwahi kuvuja miezi michache iliyopita na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kinyume na matakwa ya wahusika hatimaye leo imeweza kuachiwa rasmi, sasa kupitia kurasa ya Twitter ya Fareed Kubanda (Fid Q) ametweet...
kwa mashabiki zake kwa kuwaambia kwamba Rich Mavoko sio mtu mzuri kabisa.

Baada ya kuwafanya mashabiki wake wakae bize kutafakari unyama wa Rich Mavoko kwenye ngoma ya Sheri, shabiki mmoja wa Fid akaandika kwamba Fid amemfunika sana Rich Mavoko kwenye ngoma ya SHERI, unajua nini?, Fid Q alikanusha ile kauli na kuendelea kusisitiza kwamba Mavoko ni mtu mbaya sana.

0 comments:

Post a Comment