Pages

Subscribe:

Thursday, July 27, 2017

KAMA SI MUZIKI BASI ROSA REE ANGEKUWA NA KAZI HII HAPA


Huwezi kuwataja female rappers wanaofanya poa kinoma hivi sasa kwenye game ya music East Africa ukaacha kumtaja mwanadada Rosa Ree zao la The Industry, kutokana na hits ambazo anadropisha back to back, juhudi zake kwenye game na mambo mengine kibao. 

Leo Rosa Ree amekamata kipaza na kutusanua kitu kingine ambacho huenda angekuwa anafanya tofauti na kuwa msanii kama ambavyo wengi tunamfahamu, Rosa Ree amedai kuwa tofauti na muziki huenda angekuwa...
daktari, kutokana na chaguo ambalo alikuwa amelifanya hapo awali baada ya kumaliza kidato cha sita na kuitaka familia yake iwekeze nguvu zake katika kumpa sapoti katika sekta hiyo.

Rosa amedai kwamba alisoma kabisa masomo ya udaktari ila mwisho wa siku aliamua kuachana na harakati hizo na kuamua kufanya kile kitu ambacho anapenda (Music) na wala haikuwa shida kwa familia yake kuweza kukubaliana naye na kumpa sapoti.

0 comments:

Post a Comment