Pages

Subscribe:

Saturday, May 9, 2015

MATAPELI WAMLOSTISHA SNURA

 Matapeli Wamlostisha Snura
Staa wa Bongo Movies na Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Mama wa Majanga’ amefunguka kwa kusema kuwa mtu aliyeteka namba yake ya simu na kuitumia akiomba fedha na kuitumia kama ni yeye amemfanye apate matatizo na usumbufu usio na manufaa zaidi ya kumkera katika shughuli zake...

“Aliyenifanyia ujinga wa kuharibu namba yangu ya simu na kuanza kuitumia yeye kama mimi si siri amenitia umaskini kwa wakati ule kwani baadhi ya wateja wa kazi zangu walikuwa wakitumia kwa mawasiliano na mimi, lakini nimebadilisha namba nyingine,”anasema Snura.
Staa huyo anasema aliamua kuibadili namba yake ya simu kwani kila alipojaribu kuirudisha na kuendelea kuitumia mtu huyo aliiteka tena na kuitumia yeye bali anawasisitiza wale jamaa zake waliokuwa na namba ya zamani wasiitumie wala mtu kuwaomba fedha kupitia namba hiyo haitumii wala wasidanganywe na tapeli huyo.

0 comments:

Post a Comment