Pages

Subscribe:

Thursday, May 14, 2015

WEMA NA KAJALA WAKUTANA CLUB USO KWA USO

MAJANGA! Wasanii wawili mahasimu katika tasnia ya filamu, Kajala Masanja na Wema Sepetu ‘Madam’ wametengeneza tena vichwa vya habari baada ya kukutana ndani ya klabu ya usiku ya Maisha iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita na kuzua... minong’ono miongoni mwa wadau wengi wa burudani, Risasi Mchanganyiko linakupa hatua kwa hatua.
Matukio hayo tofauti kwa wasanii hayo yalitokea ndani na nje ya ukumbi huo katika shoo maalum ya kumchangia mke wa msanii Mabeste  Venus, Lisa Karl Fickenscher  iliyowakutanisha mastaa wengi wa ‘category’ mbalimbali.
SHUNGULI YAANZA VIZURI
Shughuli nzima ilionekana kwenda vizuri, isipokuwa mara chache ambako kulitokea vituo vya hapa na pale, ingawa vingi kati ya hivyo vilisababishwa na baadhi ya wahudhuriaji kuzidiwa na kilevi.
WATENGANISHWA
Wakati flani ‘usiku mnene’, Kajala alijongea kwenye jukwaa maalum la waalikwa (V.I.P) kutoka kujichanganya kwa wadau, ambako pia alikuwa amekaa Madam aliyeonekana kuzidiwa na ‘kiburudisho’.
Akitambua wazi kuwa lolote lingeweza kutokea, Petit Man, mtu wa karibu wa Wema, alimshika mkono na kumtoa eneo hilo, lakini muigizaji huyo alipohoji sababu za kuondolewa ‘V.I.P’, aliambiwa kuwa hapakuwa sehemu salama kwa wakati huo. 
KAJALA NDANI YA NYUMBA
Kajala alionekana akijiachia kwa mapozi na ‘mihangaiko’ ya hapa na pale ikiwemo kucheza na kubadili vinywaji akiwa sanjari na marafiki zake.Wakati wote, msanii huyo alionekana mwenye furaha iliyoambatana  na tabasamu na vicheko vya mara kwa mara jambo lililotafsiriwa kama tayari alikuwa amepata kiburudisho cha kutosha.
AKUTWA NA MKASA
Mapambazuko yalipoanza kulivamia anga, Kajala na ‘kampani’ yake walitawanyika lakini wakati wakiwa nje ghafla jamaa mmoja ambaye hakufahamika ‘aliwa-join’ na kuwachangamkia kusiko kwa kawaida huku wao wakionekana kutompa ushirikiano aliouhitaji.
AMSHIKA MAKALIO
Hata hivyo, jamaa huyo ‘alifika mbele’ zaidi kwa kumshika makalio Kajala ambaye alimnasa kibao. Katika kujibu mapigo, jamaa huyo alimpiga na chupa ya bia kichwani na kusababisha jeraha usoni.
Baada ya tukio hilo, marafiki wa pande zote mbili walijitahidi kutuliza hali ya hewa iliyochafuka na kila mmoja akaendelea na hamsini zake.
WEMA SASA
Kwa upande wake, Wema ambaye alipaswa kuwa Msema Chochote (MC) wa hafla hiyo, alipanda jukwaani kwa kusaidiwa na watu kutokana na kuzidiwa na kinywaji kisichojulikana.Baada ya kupanda, muigizaji huyo nyota alishindwa kumudu kuendelea na ratiba, kwani alizungumza maneno yasiyoeleweka na hatimaye kuishia kuwasalimu mashabiki, kitu kilichoharibu shughuli hiyo kwa jumla.
ATOKA UKUMBINI NA GLASI
Baada ya kushuka jukwaani, mmoja wa wapambe wake wa muda mrefu, Petty Man alimshika mkono na kumsindikiza hadi nje, ambako akiwa ameshikilia glasi yake ya kinywaji, Wema aliingia nayo kwenye gari, kabla ya kumwaga kilichokuwemo ndani na kumpa mtu mmoja glasi hiyo ili airudishe ndani.
Mwandishi wetu alipotaka kujua sababu ya Wema kulewa na kushindwa kufanikisha jambo muhimu, alimtaka kumuacha kwani hakuwa na muda wa mahojiano.“Tafadhali sana (akilitaja jina la mwandishi), sihitaji mahojiano, hapa nimekuja kwenye starehe, naomba uniache,” alisema Wema huku akibamiza mlango wa gari kwa nguvu na kumtaka dereva wake (Petty Man) kuondoa gari.
KUTOKA KWA WADAU
Baadhi ya watu walioshuhudia matukio ya Wema na Kajala kwa nyakati tofauti, walisikika wakisema kuwa ni kama mkosi uliowakumba wawili hao marafiki wa zamani.“Hawa bwana wana matatizo sana, wote wamekutwa na majanga kwenye eneo moja, lakini nadhani hata matatizo yao yanachangiwa sana na bifu lisilokuwa na kichwa wala miguu, wajishushe na wasameheane,” alisikika akisema mdau mmoja

0 comments:

Post a Comment