Pages

Subscribe:

Sunday, May 10, 2015

ASLAY AKABIDHIWA GARI KAMA ZAWADI YA BIRTHDAY

Mkubwa Fella amemtunuku zawadi ya Gari mwanamuziki wa Band yake ya MKUBWA NA WANAWE au "YAMOTO BAND" kama ilivyozoeleka na wengi, gari hili amepewa Aslay siku ya Birthday yake.
Kupitia kurasa yake ya mtandao wa Instagram Aslay ameshukuru kwa kusema,
"Asante mungu Kwa kunipa uhai Na kipaji ambacho leo hii kina fanya naitwa Aslay pia nakushukuru kwa kunifikisha kwenye mikono Ya mtu mwenye moyo wa kibinaadamu. Najua kuna mengi makubwa ambayo... boss wangu @mkubwafella umenifanyia ambayo si vyema kuyataja yote kwasababu wakati wake haujafikia ila naomba nichukue fulsa hii kukushukuru kwa hiki ulichonifanyia leo katika sherehe Ya kusherehekea siku yangu Ya kuzaliwa umenifanya nijione mwenye thamani kubwa duniani sikutegemea kama leo itakuwa siku yangu ya kumbukumbu ambayo sitoweza kuisahau hata Nije kuwa bilionea @mkubwafella asante kwa kunipa hii zawadi ambayo mimi kama mimi sikuiwazia kabisa kama Leo nitapata gari Na ninaushukuru uwongozi mziki Wa #mkubwanawanawe pamoja na manager wangu @chambusso boss wangu @babutale @mhtemba na mama yangu @sweatfella bila kuwasahau wasanii wenzangu wa @yamoto_band mungu ndie atakaewalipa ... "

0 comments:

Post a Comment