Pages

Subscribe:

Tuesday, April 24, 2018

JEBBY AZIKWA WASANII WATOA KIDOGO WALICHO NACHO KUFANIKISHA MAZISHI


Msanii wa Bongo Fleva, Jebby amezikwa katika makaburi ya Mailimbili mjini Dodoma. Jebby ambaye amewahi kufanya vizuri na wimbo wake wa ‘Swahiba’ alifariki dunia hapo juzi April 22, 2018 mjini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa mdogo Jebby, Hamis Omary msanii huyo hakubahatika kuwa na mke wala mtoto, pia kuna nyimbo zaidi ya...
nne alirekodi ambazo zipo tayari ila hazijatoka.

Wapili kushoto ni msanii Suma G.

Professor Jay ni miongoni mwa wasanii waliohudhuria katika msiba huo ambapo amekabidhi Tsh. 550,000 zilizochangwa na wasanii kwa ajili ya msiba huo, msanii mwingine aliyehudhuria ni pamoja na Suma G.

0 comments:

Post a Comment