Pages

Subscribe:

Wednesday, April 4, 2018

MASOGANGE KWENDA JELA MIAKA MITATU AU KULIPA MIL 1.5

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Mil 1.5 Video Queen maarufu bongo , Agnes Gerald 'Masogange' katika kesi ya kutumia dawa za kulevya . 

Masogange amepewa hukumu hiyo baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam. Hukumu ya Masogange ometolewa na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, Wilbard Mashauri ambapo amesema kuwa...
“Katika kosa la kwanza, mahakama inamhukumu kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Sh1 milioni na kwa kosa la pili, amehukumiwa kwenda jela miezi 12 au kulipa faini ya Sh500, 000".
 
Februari 17 mwaka jana, aliyekuwa Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaeleza wanahabari kuwa Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kupimwa iwapo anatumia dawa hizo za kulevya.

Awali, kabla ya kupimwa, Masogange alikamatwa na polisi akituhumiwa kutumia dawa hizo.
Mwaka 2013, alikamatwa na shehena ya kemikali bashirifu zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya, Afrika Kusini.

0 comments:

Post a Comment