Pages

Subscribe:

Tuesday, April 24, 2018

VITA YA MIAMBA YA SOKA UEFA CHAMPIONS LEAGUE KUENDELEA LEO


Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya inatarajiwa kuendelea hii leo siku ya Jumanne kwa mchezo wa kwanza wa nusu fainali kupigwa dimba la Anfield ambapo Klabu ya Liverpool itakuwa mwenyeji dhidi ya AS Roma.

Liverpool wametinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa kabisa kwa ngazi ya klabu baada ya...
kuing’oa Manchester City kwa jumla ya mabao 5-1.

 
Wakati wapinzani wao klabu ya AS Roma nao hawakupata bahati ya mtende kuingia kwenye hatua hiyo bali walilazimika kupindua matokeo mbele ya walfe wa soka wa Hispania, FC Barcelona na kuwatoa kwa faida ya bao la ugenini.
 
Rekodi ya Liverpool na AS Roma kabla ya kukutana kwenye mchezo wao wa leo wa klabu bingwa Ulaya.

Mchezo mwengine wa klabu bingwa Ulaya unatarajiwa kupigwa kesho siku ya Jumatano wakati Bayern Munich ikiwakaribisha Real Madrid ya Hispania.

0 comments:

Post a Comment