Pages

Subscribe:

Sunday, August 23, 2015

MAJIMAMA YAMWAGA RADHI MBELE YA WATOTO

JIMAMA (6)
Ama kweli dunia imekwisha! Hayo yalidhihirishwa Jumamosi iliyopita baada ya kundi la mijimama kuwamwagia radhi watoto walio chini ya umri wa miaka saba ambao walikuwa wakitolewa jandoni katika kigodoro kilichofanyika Kigogo Luhanga jijini Dar. See more pics...


JIMAMA (7)Katika kigodoro hicho kilichokesha, burudani mbalimbali kama vile muziki wa kisengeli na kigoma cha Urugway vilinogesha mkesha huo ambapo mambo yalikuwa bambam.
JIMAMA (1)Kulipopambazuka, mambo yaliendelea ambapo ilipofika saa nane mchana watoto waliotoka jandoni walitolewa uwanjani na muziki kukolea ambapo wanawake hao walioonekana kukolea kwa kilevi walijimwaya uwanjani kucheza kwa staili ya kuonesha mambo ya chumbani.
JIMAMA (2)Wamama hao walizidi kutia aibu na kuonyesha kuwa akili zao zimefyatuka baada ya dogo mmoja aliyekuwa akiwachombeza kwa rap kama za msanii Msagasumu kushika ‘mic’ na kuufanya umati uliokuwa kwenye eneo hilo upigwe butwaa.
JIMAMA (3)Minenguo na mikogo ya mijimama hiyo ilisababisha baadhi ya waungwana waliokuwa kwenye shughuli hiyo kufumba macho na wengine kuondoka kabisa wakieleza kuwa kilichokuwa kikifanyika ni kinyume na maadili.
JIMAMA (5)“Hee, hawa akinamama watakuwa wamelaaniwa, ndiyo nini sasa kufanya haya mambo ya chumbani mbele za watoto? Huu siyo ustaarabu kabisa,” alisema mzee mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja.

0 comments:

Post a Comment