Pages

Subscribe:

Sunday, August 16, 2015

STORY: PETE YA JINI SABRAH EPISODE-1


PETE YA JINI SABRAH - 1 
Mtunzi : Mwinyimvua Rajabu
 0789 569355
Kwa jina naitwa Saidi ni kijana wa wastani tu wa miaka kadhaa naishi jijini dar es salaam maeneo ya vingunguti sokoni mimi ni mjasilia mali wa kawaida tu hapa jijini dar es salaam nakumbuka siku moja ilikuwa kama saa 4 usiku hivi wakati narejea nyumbani njiani nilikuta ugomvi mkubwa sana vijana wawili wakilumbana kwa kutupiana matusi sikujua chanzo cha ugomvi ule niliji sogeza taratibu katika kundi lile la watu waliokuwa...
wakiwa tazama vijana waliokuwa wakilumbana nilimsikia kijana mmoja kati ya waliokuwa wakigombana akimwambia mwenzake kuwa " ipo siku atamuua tu ".

Kiukweli ugomvi ule nilipojaribu kuulizia chanzo cha kulumbana shuhuda mmoja akaniambia kuwa "chanzo cha ugomvi ule wanagombania mwanamke " Kwa kuwa ilikuwa usiku sana giza likichukuwa nafasi yake pamoja na uchovu wa kazi niliokuwa nao mchana kutwa niliondoka taratibu kuelekea nyumbani huku nyuma nikiacha ule ugomvi ukiendelea haikuchukua muda mrefu kufika nyumbani haraka niliingia ndani kitu cha kushangaza hali niliyoikuta chumbani kwangu ilikuwa tofauti kabisa na nilivyoi acha asubuhi.

kutokana na uchovu niliokuwa nao sikuitilia maanani hali ile nilivua nguo zangu na kujirusha kitandani kama mzigo wa kuni usingizi ulichukuwa nafasi yake muda ule masaa yalikatika sekunde zikiyoyoma nje sauti za mbwa zilisikika zikibweka usiku ule jijini dar es salaam hasa maeneo ya vingunguti kusikia sauti za mbwa wakibweka ni kawaida tu ndoto za ajabu zilijia pasipo kujua zina maanisha nini miongoni mwa ndoto niliyo ota ilikuwa hivi " niliota nipo beach na marafiki zangu tukipunga upepo gafla..." 

ITAENDELEA SIKU YA JUMATANO

Story hii itakujia kila siku ya J-Pili na J-Tano

0 comments:

Post a Comment