Pages

Subscribe:

Sunday, August 30, 2015

Q-CHIEF: MWANANGU ALIFUKUZWA SHULE KISA ALIMPIGA MWENZAKE BAADA YA...

10956351_663821843741171_1618248528_n
Q Chief amedai kuwa aliumia mno pale mtoto wake alipofukuzwa shule baada ya kupigana na mwanafunzi mwenzake aliyemtania kuwa baba yake ni teja! Q-Chief alikuwa akizungumza na BBC Swahili hivi karibuni. Na kusema kuwa...
 
1391193_700453833312677_2145510502_n
Mtoto wa Q Chief
“Siku moja mwanangu alikuja analia sana, akaniambia baba mwanafunzi mmoja amesema baba yake si teja tu. Nikamwambia kwahiyo ukafanyaje akaniambia ‘nimempiga ndio maana nimefukuzwa’, nikamuuliza ‘kwanini umempiga?’ akasema nimejisikia uchungu sana,” alisema.
“Kwahiyo nikaona kama mtoto wa miaka tisa anaweza kusikia uchungu, amenyimwa haki zote za malezi ya baba. Nikajiuliza sio watu wote wananijali zaidi lakini huyu ni doctor kesho au ni lawyer au atafanya kazi BBC, napaswa kuwa mfano mzuri kwake, nikaamka asubuhi nikasema inatosha.”

0 comments:

Post a Comment