Pages

Subscribe:

Sunday, August 23, 2015

STORY: PETE YA JINI SABRAH.. EPISODE-3


PETE YA JINI SABRAH - 3 
Mtunzi : Mwinyimvua 
0789 569355 

Taratibu akaingia chumbani kwangu mama sophia huku akionekana kama mtu mwenye hofu kubwa moyoni. " vipi tena shemeji mbona usiku kuna nini?? " Nilimuuliza mama sophia huku nikivaa shati langu " Shemeji mume wangu kazidiwa gafla anaumwa hali yake mbaya naomba msaada wako " Mama sophia alisema.

Huku akibubujikwa machozi Nilitoka upesi chumbani kwangu na mama sophia kuelekea chumbani kwa mama sophia haraka sikuamini nilichokikuta nilimkuta...
baba sophia akitokwa mapovu mdomoni huku puani na masikioni akitokwa damu nilijikaza kiume nikachukua kitambaa kumpangusa zile damu na mapovu mwanaume mwenzangu huku mama sophia alisikika akilia kwa huzuni kubwa juu ya hali ya mumewe aliyokuwa nayo kipindi kile.

" Mama sophia nenda upesi kamu amshe fredy " Sauti yangu ilisikika nikimwambia mama sophia haikuchukua muda mrefu fredy na mama sophia walifika pale chumbani nilipokuwa mimi " Saidi saidi kuna nini tena??? " Sauti ya fredy ilisikika ikiniuliza " Mimi sijui chochote fredy " Nilimjibu fredy Kipindi chote wakati tupo mule ndani kwa mgonjwa wazo la haraka lilitujia mimi na fredy juu ya kumpeleka hospitali mama sophia kwa mbali alisikika akisema " Hospitali gani saizi saa 8 usiku ipo wazi ??? " "

Tumpelekeni amana hospital jamani hali inazidi kuwa mbaya " Fredy alisema huku akielekea chumbani kwake upesi kuchukua akiba ya pesa na funguo za taksi haikuchukua muda mrefu tulitoka upesi Kuelekea Amana hospital huku fredy akiendesha gari kwa speed ya hali juu kiza kikubwa tulikikata kuelekea amana huku mama sophia akionekaa akilia.

kipindi chote hiko baba sophia bado akiwa mikononi mwangu damu na mapovu yakizidi kumtoka sikuweza kuamini gafla... Itaendelea Jumatano

0 comments:

Post a Comment