Msanii wa muziki wa Hip Hop bongo Roma Mkatoliki amefungiwa kufanya
shughuli za muziki kwa muda wa miezi sita kwa kile kilichodaiwa msanii
huyo kudharua wito wa BASATA na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo.
Akiongea na waandishi wa habari Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Juliana Shonza amesema kuwa amechukua maamuzi hayo kutokana na kumwita msanii huyo ili aweze kufika kwenye mkutano huo lakini...
hakuweza kufika wala hakutoa taarifa yoyote ile.
"Roma Mkatoliki alipigiwa simu na BASATA hapokei na anatumiwa message anasoma lakini hajibu kitu, kwa hiyo kimsingi hilo ni kosa kwa sababu tumemuita si kama tumekurupuka bali Roma Mkatoliki aliutoa wimbo wake muda kidogo unaitwa Kibamia kimsingi ule wimbo ameimba matusi matupu na ni wimbo ambao kiasi fulani unadhalilisha kwa sababu mtu unapozungumzia kibamia huitaji kujiuliza kibamia ni nini kila mtu anajua maana ya kibamia, mimi siamini hata mtu ambaye yupo hivyo anakuwa amependa"
Juliana aliendelea kutoa ufafanuzi kuhusu suala la Roma Mkatoliki
"Nakumbuka mwaka jana nilikuagiza Mkurugenzi wa BASATA kwamba umwite Roma Mkatoliki ukae naye chini, kwenye onyo lake la kwanza mwambie afanyie marekebisho huo wimbo na uzuri BASATA walimwita wakaa naye chini wakamwambia kasoro za wimbo wake na kutakiwa kufanya marekebisho ya wimbo huo ikiwepo jina lenyewe la Kibamia, pamoja na baadhi ya matusi ambayo yapo kwenye huo wimbo. Roma Mkatoliki alikubali na kusema ataenda kufanyia marekebisho hizo sehemu cha kusikitisha mpaka saizi napoongea hakuna ambacho kimefanyika na mbaya zaidi wimbo huo unaendelea kupigwa kwenye vyombo vya habari"
"Roma Mkatoliki amedharau maagizo ambayo alipewa na BASATA na kwa sababu tumemwita leo na hajafika bila taarifa yoyote hivyo amedharau wito, mimi kama Naibu Waziri wa Habari pamoja na BASATA tumekubaliana kwamba huyu ndugu Roma Mkatoliki tunampa adhabu kwa mujibu wa Katiba na kanuni, hivyo tunamfungia kwa muda wa miezi sita ndani ya muda huo wa miezi sita hakuna kufanya kazi yoyote ya sanaa, hakuna kutoa wimbo wowote, hakuna kufanya show sehemu yoyote, huo wimbo moja kwa moja tunaufungia" alisisitiza Shonza

0 comments:
Post a Comment