Pages

Subscribe:

Thursday, March 29, 2018

MR NICE: SIMKUBALI MSANII YEYOTE NAJIKUBALI MI MWENYEWE


Msanii wa muziki Bongo, Mr. Nice amedai kuwa hamkubali msanii yeyote zaidi yake hata akipewa fursa ya kutaja orodha ya wasanii watano anaowakubali nafasi hizo zote atajipatia yeye.

Muimbaji huyo aliyetamba na style ya Takeu amesema hayo nchini Rwanda alipokuwa akifanya show weekend iliyomalizika. Mr Nice amewataja wasanii...
anaowakubali ni Lady Jaydee, Professor Jay na Jose Chameleone kutoka nchini Uganda.

“Lady Jaydee ni legendari mwenzangu, ni wanamuziki mwenzangu, hivyo hivyo kwa Professor Jay,” amesema.

“Jose Chameleone is Friend of mine ambaye ninaweza nikavua viatu vyangu nikamwambia vaa Jose, dah huyu mtu unajua mimi simkubali mwanamuziki yeyote, namkubali Mr. Nice tu ukiniambia nikupe top five yangu msanii wangu nitakuambia ni Mr. Nice,” amesisitiza.

Mr. Nice kwa sasa anafanya vizuri na ngoma inayokwenda kwa jina la Tuheshimiane.

0 comments:

Post a Comment