Pages

Subscribe:

Saturday, March 17, 2018

FAHAMU KITU KUHUSU HII CHOCOLATE YA GHARAMA KULIKO ZOTE DUNIANI

Inawezekana wewe ni moja kati ya watu wanaopenda chocolate kama kitafunwa (snack) lakini je umewahi kuhisi kuna chocolate ya gharama ya juu zaidi kiasi cha kupelekwa kwenye maonyesho ya biashara?.

Basi jana March 16, 2018 chocolate inayodaiwa kuwa ya gharama ya juu zaidi duniani ilipelekwa kwenye maonyesho ya biashara kwenye Mji wa Obidos nchini Ureno.
Chocolate hiyo ambayo ni ya gharama ya Euro 7,728 ambayo ni sawa na Fedha za Kitanzania Shilingi Milioni 20.7, imefunikwa na...
dhahabu inayoweza kuliwa, na imetengenezwa na vitu vingine ikiwa ni pamoja na truffle nyeupe, nyuzinyuzi za saffron, na vanilla kutoka Visiwa vya Madagascar.

Mtengenezaji wa chocolate hiyo Daniel Gomes ambaye ni raia wa Ureno ameeleza kuwa chocolate hiyo ambayo ina umbo la fedha imepewa cheti cha kutambuliwa kama Chocolate ya gharama ya juu zaidi duniani na Kitabu cha Kumbukumbu cha Guiness mwaka 2017.

0 comments:

Post a Comment