Pages

Subscribe:

Thursday, March 29, 2018

JUX: IKIFIKA WAKATI WATU WATAJUA HATUWEZI KUFICHA UJAUZITO

Jux ameeleza hayo wakati alipokuwa anahojiwa na moja wapo ya chombo cha habari nchini Tanzania baada ya kuenea picha ya mpenzi wake Vanessa mitandaoni ikiwa inamuonesha tumbo lake limeja jaa mithiri ya ujauzito.

"Kiukweli Vanessa hana ujauzito ile ni picha tu, labda siku hiyo alikuwa ametoka kula 'ameshiba' na kupigwa picha vibaya ndio ikatokea hivyo. Lakini hakuna kitu kama hicho, hivyo vitu inabidi...
viende kwa mipango pia lazima mwenzako umshirikishe endapo unataka kufanya hivyo na mkubaliane ili mambo yaweze kwenda sawa", amesema Jux.

Pamoja na hayo, Jux ameendelea kwa kusema "ikifika 'time' watu watajua kwasababu sisi hatuwezi kuficha mambo hata kama sisi hatuto-post lakini inaweza akaja ku-post mtu mwingine kwa kutuona sehemu fulani".

Jux kwa sasa anafanya vizuri kibao chake kipya kilichopewa jina la 'fimbo' aliyoachia siku za hivi karibuni.

0 comments:

Post a Comment