Pages

Subscribe:

Thursday, January 7, 2016

AMINI KUTOA AUDIO 24 NA VIDEO 24 MWAKA HUU

amini


Msanii wa muziki, Amini ameweka wazi mipango yake mipya ya mwaka huu kwenye muziki wake.

Miongoni mwa mambo ambayo amepanga kuyabadilisha kwenye utaratibu wake wa kufanya muziki ni kuongeza idadi ya nyimbo ambazo huachia kwa mwaka mzima.

“Plan zangu za kwa 2016 ziko tofauti kidogo na 2015, kwasababu 2015 nilikuwa natoa nyimbo kwa kusikilizia labda wimbo mmoja unaweza...
ukakaa mwaka mzima.” Alisema Amini kwenye mahojiano na Bongo5.

“Lakini kwa 2016 kila mwezi nitakuwa natoa nyimbo mbili kila mwezi kutokana na nyimbo nyingi nimezirekodi ambazo ziko katika benki yangu. Kwahiyo 2016 nitakuwa natoa nyimbo mbili kila mwezi kwa nafasi lakini sio mfululizo, na kuhakikisha nyimbo zote zitakuwa zinapata video.” alisema Amini. Hivyo tutegemee kupata nyimbo 24 pamoja na video zake kwa mwaka huu mzima.

Amini amesema kuwa nyimbo atakazokuwa anatoa zitakuwa na mahadhi tofauti ili kuwaburudisha mashabiki wengi zaidi.
Upande mwingine Amini amesema kuwa hafikirii kutoa album mwaka huu licha ya kuwa na nyimbo nyingi ambazo zingetosha kutoa album, mpaka pale mifumo ya soko la album itakapokaa sawa.

0 comments:

Post a Comment