Pages

Subscribe:

Friday, January 8, 2016

MBWANA ALLY SAMATA ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA

Mwana Samatta Glo
Hatimaye matarajio na matumaini ya mamilioni ya watanzania yametimia, Mbwana Ally Samatta ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya bara la Afrika.

Usiku wa January 7, 2016 umekuwa mtamu sana kwa Samatta na watanzania kwa ujumla kutokana na kijana huyo wa Mbagala kuiletea Tanzania heshima kubwa kwenye sekta ya michezo hususan soka. Samatta alikuwa akipambana na...

wachezaji wengine wawili ambao ni Robert Kidiaba Muteba (DR Congo & TP Mazembe) na Baghdad Bounedjah (Algeria & Etoile du Sahel).

Msemo wa wahenga kwamba ‘nyota njema huonekana asubuhi usemi huo’ ulianza kujitokeza mapema pale ambapo jina la nyota huyo wa Afrika lilipojitokeza kwenye list ya majina ya wachezaji wanaounda kikosi bora cha wachezaji wa Afrika.

Pierre-Emerick Aubameyang amenyakua tuzo ya mchezaji bora Afika 2015 na kumpiga chini Yaya Toure ambaye ni mshindi mara nne mfululizo wa tuzo tuzo hiyo na alikua anaitetea tena kwa mara nyingine lakini ameshindwa kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo hiyo mara tano.

samatta2
Mbwana Ally Samata kushoto Akiwa na Pierre aubameyang upande wa Kulia


Ukiachana na tuzo ambayo ilikuwa inasubiliwa kwa hamu na mashabiki wengi wa soka duniani kote ambayo ni tuzo ya mchezaji bora wa Afrika yenye vipengele viwili kipengele cha kwanza ni mchezaji bora wa Afrika kwa ujumla na kipengele cha pili ni mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Afrika) kuna tuzo mbalimbali zilitolewa kwa washindi.

Haya ni majina ya washindi wa tuzo mbalimbali zilizotolewa usiku wa January 7, 2016

Timu bora ya taifa ya mwaka kwa upande wa wanaume: Ivory Coast
Timu bora ya taifa ya mwaka kwa upande wa wanawake: Cameroon
Kocha bora : Herve Renard (aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Ivory Coast)
Mchezaji bora kijana: Victor Osimhen (Nigeria)
Mchezaji bora chipukizi:Etebo Oghenakoro (Nigeria)
Fair play award (mchezaji muungwana): Allez Casa (Senegal)
Klabu bora ya mwaka: TP Mazembe
Mchezaji bora wa kike: Gaelle Enganamouit (Cameroon)
Mwamuzi bora wa mwaka: Papa Bakary Gassama (Gambia)
Wachezaji wakongwe: Charles Kumi Gyami (Ghana) na Samuel Mbappe Leppe (Cameroon).


0 comments:

Post a Comment