Pages

Subscribe:

Tuesday, January 19, 2016

T.I.D AMSAINI KR KWENYE LEBBO YAKE YA RADAR ENTERTAIMENT

KR akiwa na TID


CEO wa Radar Entertainment, TID amesema ameamua kumsaini rapa wa zamani wa Wanaume Family, KR Mullah kwa kuwa ameona ana kitu cha ziada ambacho wasanii wengine hawana.

Akizungumza katika kipindi cha Friday Night Live cha EATV, TID alisema wakati yupo tour na KR, alishangaa kuona msanii huyo akipapatikiwa na mashabiki kuliko wasanii wengine.

“KR nilikutana naye kwenye tour ya mheshimiwa Majaliwa. Sasa wakati tunatoka Dar es salaam tumefika Lindi KR alikuwa amekaa...
dirishani tupo wasanii kibao lakini kila sehemu tukisimama KR, KR , KR Mullah. Nikasema kuna wasanii zaidi ya 15 lakini KR ndiye anayeoneka!!

Nikasema huyu naweza kumsaidia kwa sababu ana kipaji. Mimi KR nilikuwa namuona ITV wakati nipo shule, kwahiyo ni msanii ambaye bado ana impact kubwa sana kama akipewa support,” alisisitiza TID.
Pia TID amewataka mashabiki wake kusubiria project za KR akiwa Rader pamoja mixtape ya Radar Entertainment.

0 comments:

Post a Comment